Mimi nilikuwa namiliki Mitsubishi Pajero Mini, ambayo haina tofauti kubwa sana na Pajero Jr. Tatizo la hapa bongo ni kwamba, magari ya Mitsubishi yanahitaji umakini wa hali ya juu katika kuyatengeneza, si rahisi kama gari za Toyota. Mafundi, kama unavyowajua, huwa hawakubali kushindwa, hatimaye wanakuingiza hasara. Unatoa pesa nyingi, unatengeneza gari, mwisho wake inagoma, inaharibika, unaingia hasara, na kwa hasira, wala hutaki kumwona fundi aliyekuingiza mjini.
Suala la Cami halina ubishi. Ni gari isiyo na utata. Mwanzoni watu walilalama kwamba hakuna spare, lakini hicho kinatokana na (a) kutokujua kwa watu wanaojifanya wajuaji, na (b) ubabaishaji, ili mradi aonekane anajua, kumbe hajui.
Cami gari nzuri sana, haitakupa shida. Spare zipo na ni rahisi kuitengeneza.