Miss wa Lundenga ashiriki shindano nje kinyemela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miss wa Lundenga ashiriki shindano nje kinyemela

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Simba Mkali, Aug 23, 2012.

 1. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 593
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  MISS aliyetwaa nafasi ya 2, 2012 katika shindano maalum la mwaka huu, Hamisa Hassan, anadaiwa kuichafua Miss Tanzania kufuatia kwenda kushiriki kinyemela Shindano la Miss University Africa 2012 nchini Nigeria hivi karibuni.
  Ilidaiwa kuwa ili mrembo ashiriki shindano hilo, linalopokea walimbwende kutoka barani Afrika, lazima atoke kwenye moja ya vyuo vya nchini mwake sifa ambayo Hamisa hakuwa nayo.
  Ilibidi mapaparazi wetu wamsake Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Anko’ ili atoe ufafanuzi kuhusu madai hayo hasa ikizingatiwa kuwa, katika shindano maalum la hivi karibuni, Lissa Jensen aliibuka kidedea na Hamisa kushika nafasi ya pili.
  “Ni kweli Hamisa ni miss wangu, lakini utaratibu wa kwenda Nigeria kushiriki shindano hilo sifahamu aliutoa wapi? Najua hakuna chuo chochote anachosoma kwa sasa na wala hakuna mashindano kama hayo kwangu,” alisema Lundenga.
  Kwa upande wake, Hamisa alipobanwa ili kutoa maelezo kuhusu tuhuma hizo alikiri kutosoma chuo chochote nchini.
  Aidha, alikiri kushiriki shindano hilo huku akisema kuwa hayupo tayari kuwataja waliomchagua.
  “Ni kweli sisomi chuo chochote ingawa nina mpango huo, ni kweli nilikuwa Nigeria kushiriki Miss University Africa 2012 na niliingia top ten, lakini taji lilichukuliwa na mshiriki kutoka Lesotho (pichani chini), lakini siwezi kuwataja walionichagua kwenda,” alisema. MISSSSSSSSSSSSSSS.jpg
   
 2. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Huyu binti nilimuona tangu akiwa mdogo. Ni kweli ana ambitions kubwa ila moto wake anaoenda nao ataishia kama watu fulani fulani tunawajua!
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Kwani huyu binti ameajiliwa na Lundenga ndio kwamba kila atakachofanya apate ruhusa ya Lundenga? huu ni upuuzi mtupu hakuna story hapa zaidi ya uandishi njaa.
   
 4. c

  christmas JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,606
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  hahaahaha!
   
 5. deejo

  deejo Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Sikapendi haka katoto. Kanatafuta umaarufu kwa nguvu km Lulu wa Kanumba.Halafu role model wake ni Wema sepetu. PATA PICHA! Sijui kataishia wapi tufuatilie hii tamthilia yake,,,yasije kuwa ya km ya Lulu
   
Loading...