Misri na Sudan kuanza mazoezi ya kijeshi ya pamoja dhidi ya Ethiopia

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Misri na Sudan kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kukabiliana na Ethiopia

Nov 15, 2020 08:11 UTC


Majeshi ya Misri yametoa taarifa kuhusu mpango wa kufanyika luteka na mazoezi ya pamoja ya anga ya kijeshi kati ya nchi hiyo na Sudan katika anga ya Sudan.

Gazeti la al Ahram la Misri limenukuu taarifa ya majeshi ya nchi hiyo ikisema kwamba askari wa jeshi la anga la Misri jana Jumamosi waliwasili katika kituo cha kijeshi cha Meroë nchini Sudan kwa ajili ya mazoezi hayo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, luteka na mazoezi hayo ya kijeshi yamepewa jina la "Tai wa Mto Nile 1" na yatafanyika kwa kushirikiana na jeshi la anga la Sudan. Maneva hayo yataendelea hadi tarehe 26 mwezi huu wa Novemba.

Mazungumzo ya pande tatu za Ethiopia, Misri na Sudan kuhusu bwawa la al Nahdha

Mazoezi ya kijeshi baina ya vikosi vya naga vya Sudan na Misri yanafanyika huku kukiwa na mzozo baina yao na nchi jirani ya Ethiopita kuhusu ujenzi wa bwawa la al Nahdha nchini Ethiopia. Wachambuzi wanasema, huo ni ujumbe maalumu wa Cairo na Khartoum na serikali ya Addis Ababa.

Karibu mwaka mzima sasa nchi hizo tatu zina mzozo kuhusu bwawa hilo. Mzozo huo umekuwa mkubwa kiasi cha kupiga kengele la hatari na kuongeza uwezekano wa kushambuliwa kijeshi bwawa hilo. Serikali ya Ethiopia imepiga marufuku ndege kuruka katika anga ya eneo la bwawa hilo na imeshadidisha ulinzi ikisisitiza kuwa imejiandaa kwa hali yoyote ile.

Mazungumzo baina ya nchi hizo tatu yameshafanyika mara chungu nzima bila ya mafanikio. Misri inadai kuwa bwawa la al Nahdha litapunguza kiwango cha maji ya Mto Nile yanayoelekea Misri, wakati Ethiopia inajitetea kwa kusema, ina haki ya kutumia rasilimali za nchi yake kuwaletea watu wake maendeleo na ustawi.

My take:Hawa wasudan na wamisri wanatumwa na nani?kwanini diplomasia isichukue mkondo wake na kwani Ethiopia hawana haki ya kufaidika na maji?
 
Ethiopia's prime minister has said his country "will not cave in to aggressions of any kind" after President Donald Trump suggested Egypt could destroy a controversial Nile dam.

The Grand Ethiopian Renaissance Dam is at the centre of a long-running dispute involving Ethiopia, Egypt and Sudan.

Mr Trump said Egypt would not be able to live with the dam and might "blow up" the construction.

Ethiopia sees the US as siding with Egypt in the dispute.

The US announced in September that it would cut some aid to Ethiopia after it began filling the reservoir behind the dam in July.
On Saturday, Ethiopia's foreign minister summoned the US ambassador to clarify President Trump's comments.

Why is the dam disputed?​

Egypt relies for the bulk of its water needs on the Nile and is concerned supplies could be cut off and its economy undermined as Ethiopia takes control of the flow of Africa's longest river.
Once complete, the $4bn (£3bn) structure on the Blue Nile in western Ethiopia will be Africa's largest hydro-electric project.
The speed with which Ethiopia fills up the dam will govern how severely Egypt is affected - the slower the better as far as Cairo is concerned. That process is expected to take several years.
  • Who owns the River Nile - and why it matters
  • Egypt fumes as Ethiopia celebrates over Nile dam
  • How the Nile's mega dam will be filled
Sudan, farther upstream than Egypt, is also concerned about water shortages.
Ethiopia, which announced the start of construction in 2011, says it needs the dam for its economic development.
Negotiations between the three countries were being chaired by the US, but are now overseen by the African Union.

What did the Ethiopian PM say?​

PM Abiy Ahmed did not address Mr Trump's remarks directly, but there appears to be little doubt what prompted his robust comments.

Ethiopians would finish the dam, he vowed.
"Ethiopia will not cave in to aggression of any kind," he said in a statement. "Ethiopians have never kneeled to obey their enemies, but to respect their friends. We won't do it today and in the future."

Threats of any kind over the issue were "misguided, unproductive and clear violations of international law".

In a separate statement, the foreign ministry said: "The incitement of war between Ethiopia and Egypt from a sitting US president neither reflects the longstanding partnership and strategic alliance between Ethiopia and the United States nor is acceptable in international law governing interstate relations."

Source:
BBC
 
Ethiopia anapitia kipindi kigumu sana, migogoro ya ndani mara kudhorota kwa uchumi.

Kwa ushauri aepukane na huu mgogoro maana kama ataingia vitani ayaenda kushindwa.
 
Hivi huu mtu Nile si unaanzia Ziwa Victoria kwa nini na sisi tusitengeneze Bwawa kubwa kwa ajili ya kusambaza maji ya kunywa kata ya ziwa mpk Dodoma.

Maana sisi wenye asilimia kubwa kwenye hilo ziwa hatufaidiki nalo, ila wengine huko wanatoana roho na sisi tumekaa tu kizembe
 
Egypt wasiwatishe wenzao kwani hata wenyewe wana bwawa lao la Aswan High Dam ambalo linaweza pia likalipuliwa na Ethiopia, Ethiopia nao hawako vibaya kijeshi kiasi cha kutishiwa na mtu.
 
Hivi huu mtu Nile si unaanzia Ziwa Victoria kwa nini na sisi tusitengeneze Bwawa kubwa kwa ajili ya kusambaza maji ya kunywa kata ya ziwa mpk Dodoma

Maana sisi wenye asilimia kubwa kwenye hilo ziwa hatufaidiki nalo.. ila wengine huko wanatoana roho na sisi tumekaa tuu kizembe
Tumeshaanza, maji teyari yameshavutwa mpaka tabora pia kunampango wa kuyapeleka Dodoma.
 
Nasikia
Hivi huu mtu Nile si unaanzia Ziwa Victoria kwa nini na sisi tusitengeneze Bwawa kubwa kwa ajili ya kusambaza maji ya kunywa kata ya ziwa mpk Dodoma

Maana sisi wenye asilimia kubwa kwenye hilo ziwa hatufaidiki nalo.. ila wengine huko wanatoana roho na sisi tumekaa tuu kizembe
Nasikia Mwl Nyerere alifatwa na Israel wakamwambia wanataka waya divege Maji ya ziwa victoria yanayomwagika mto Nile kuyaleta kanda ya kati haswa dodoma Kwa gharama sao wenyewe ili kupunguza kiwango cha Maji MTO Nile kuwakomoa waarabu maana MTO Nile wanautegemea Sana nasikia Nyerere akakataa ofa aliyopewa kwa kuleta ujamaa wake kuwaonea huruma waarabu na ndo chanzo cha tz kutokua na uhusiano wenye tija na Israel hata ubalozi wao haupo hapa nchini.
 
Back
Top Bottom