Misri kuipiga Ethiopia?

Misri kuipiga Ethiopia?

Unajua ni common sense kama mto umepita kwangu lazima maji niyatumie otherwise utoe huo mto
Huu ubabe wa Egypt ni upuuzi tuu Wahabeshi komaeni mpaka kieleweke!
 
nile.jpg
 
Japo mto Nile ni chanzo muhimu sana cha maji kwa Wamisri, kinachonikeraga mara nyingi ni kitendo cha Egypt kuona wao peke yao ndiyo wenye haki ya kuyatumia hayo maji na wengine wasiyaguse kabisa. Ethiopia wameonesha mfano mzuri sana kwa kuvunjilia mbali mkataba wa kionevu na kikandamizaji, huwezi kufa na kiu wakati maji unayaona mbele yako kisa mkataba wa kikoloni ,huo ni ujinga.
 
ITV Tanzania
Bunge la Ethiopia, limefutilia mbali
mkataba uliosaniwa wakati wa utawala
wa kikoloni, ulioipa Misri na Sudan, haki ya
kutumia maji mengi ya mto Nile. Serikali ya Ethiopia, imehoji kuwa
mkataba huo ulioidhinishwa mwaka wa
1929, umepitwa na wakati. Serikali ya Misri, imepinga vikali hatua hiyo
na imekasirishwa na uamuzi wa Ethiopia
wa kujenga bwawa la maji, katika mto
huo wa Nile, ikidai kuwa itapunguza maji
yake.
Siku ya Jumatatu rais Mohamed Morsi,
alisema hataki vita, lakini anachunguza
njia zote.

Bunge la Tanzania Limeshindwa nini kuvunja Mikataba ya Kifisadi serikali inayosaini?????????

OMBI MAALUMU:
Naomba Mods msipeleke hii mada jukwaa la Kimataifa,ina Maslahi ya Kitaifa na hapa ndipo watu wengi wanaiona!
Naunga mkono uamuzi wa Ethiopia, kwa kuwa hawakutawaliwa kama kina sie wengine kwani babu gamba alishasema kuwa UKIWA NA WARIDI NAWE LAZIMA UNUKIE HARUFU NZUUUUURIIII YA UA WARIDI
'All popular movements. They are the volcanic eruptions of human passions and emotions, stirred into activity by the ruthless Goddess of Distress or by the torch of the spoken word cast into the midst of the people"
 
embu nijuze kwa nini ethiopia haiwezi kuchapwa na egypt,.
Ni pm nisome vizuri.
Tnx

Sina haja ya kuku-pm ila kama unavyojua uhusiano uliopo kati Ethiopia na Israel ni kama mtu na ndugu yake na uhasama uliopo kati ya Misri na Israel ni kama binadamu na nyoka. Vita ya Misri na Ethiopia ni kama kusema itakuwa vita ya Israel na Misri na hapo nadhani unaelewa namaanisha nini..Misri atasaidiwa na Waarabu wote na Israel kama kawaida atakuwa na US backing......hadi hapo changanua mwenyewe ujue nini kitatokea......Israel anatafuta sana namna ya kupima uwezo wake na Waarabu kijeshi na proxy war ambayo atapiganisha Ethiopia na Egypt itakuwa fursa nzuri kwake kudhihirisha uwezo wake.

Egypt wanajua hilo na kamwe hawatataka vita na Ethiopia.......pia ujue Ethiopia ni moja ya nchi zenye uwezo mkubwa sana wa kivita hata bila msaada wa Israel
 
Ethiopians sio kama sisi watz na ndio maana ukiangalia hata kwenye Vitabu Vitakatifu wameandikwa mara nyingi zaidi!
Baadhi ya maamuzi magumu waliyowahi kuyafanya ni:

  • Kuvunja Muungano wa Asmara na Addis
  • Kuweza kuendesha shirika lao la ndege kwa ufanisi
  • Ushawishi wa kuwa makao makuu ya Afrika
Sisi tunashidwa hata kumwajibisha waziri sembuse kuvunja mikataba ya mabwana wakubwa!
 
ngoja wazichape tuone! ila lazima misri wakomae manake wakicheza tu ethiopia akaanza kutumia hayo maji basi nchi nyingine zote zinaanza nazo kutumia hayo maji bila woga tena.. naomba sana iwe hivo manake hawa waarabu koko wamezidi sana kujifanya wanajua ilihali hakuna ki2!!
 
Sina haja ya kuku-pm ila kama unavyojua uhusiano uliopo kati Ethiopia na Israel ni kama mtu na ndugu yake na uhasama uliopo kati ya Misri na Israel ni kama binadamu na nyoka. Vita ya Misri na Ethiopia ni kama kusema itakuwa vita ya Israel na Misri na hapo nadhani unaelewa namaanisha nini..Misri atasaidiwa na Waarabu wote na Israel kama kawaida atakuwa na US backing......hadi hapo changanua mwenyewe ujue nini kitatokea......Israel anatafuta sana namna ya kupima uwezo wake na Waarabu kijeshi na proxy ya ambayo atapiganisha Ethiopia na Egypt itakuwa fursa nzuri kwake kudhihirisha uwezo wake.

Egypt wanajua hilo na kamwe hawatataka vita na Ethiopia.......pia ujue Ethiopia ni moja ya nchi zenye uwezo mkubwa sana wa kivita hata bila msaada wa Israel

Mkuu kwani ule mkataba wa amani kati ya Israel na Misri si bado upo?
 
Mkuu kwani ule mkataba wa amani kati ya Israel na Misri si bado upo?

Ukitaka kujua tabia ya Israel angalia waliifanya nini Mv Marmara ya Uturuki....wakati Israel na Turkey ni long time friends na wana uhusiano wa kijeshi....jamaa wanaangalia maslahi yao tu na si vinginevyo. Akipata chance ya kui-destabilize Egypt atafanya hivyo mara moja. Egypt naye anajua hawezi fanya vita na Ethiopians....

......pia kaa ukijua Israel alikuwa na mchango mkubwa sana katika kuhakikisha South Sudan inajitenga toka Khartoum alisaidia sana waasi kina Gen Garang...na yote hiyo ilikuwa kumkomesha Sudan na Egypt.....hiyo vita itakuwa kubwa kuliko unavyodhani.
 
Egypt is just bluffing, owing to her military superiority they are using this tramp card just to scare others. I don't think their threats of war are real.
 
Sina haja ya kuku-pm ila kama unavyojua uhusiano uliopo kati Ethiopia na Israel ni kama mtu na ndugu yake na uhasama uliopo kati ya Misri na Israel ni kama binadamu na nyoka. Vita ya Misri na Ethiopia ni kama kusema itakuwa vita ya Israel na Misri na hapo nadhani unaelewa namaanisha nini..Misri atasaidiwa na Waarabu wote na Israel kama kawaida atakuwa na US backing......hadi hapo changanua mwenyewe ujue nini kitatokea......Israel anatafuta sana namna ya kupima uwezo wake na Waarabu kijeshi na proxy war ambayo atapiganisha Ethiopia na Egypt itakuwa fursa nzuri kwake kudhihirisha uwezo wake.

Egypt wanajua hilo na kamwe hawatataka vita na Ethiopia.......pia ujue Ethiopia ni moja ya nchi zenye uwezo mkubwa sana wa kivita hata bila msaada wa Israel

sure,ni kweli unachoongea,
nakumbuka walivyo isambaratisha al shababu kipindi kile,pia katika vita vya pili vya dunia mu italy alishindwa vibaya,
ni nchi pekee ambayo haikutawaliwa Africa.
 
Juzi Museven nae akikaririwa na BBC ametoa tamko kuhusiana na kauli ya Misri. Amesema Misri wasirudie makosa ya serikali za nyuma za kuutumia mkataba na uingereza ambao waliingia wao na uingereza pekee kuzishinikiza nchi zinazopitiwa na Nile. Amwsema hilo litakuwa kosa kubwa kwani nchi zote zina haki sawa ya kunufaika na Nile.
 
Back
Top Bottom