Misitu kaeni mkao wa kula- ulaji huoooooo!

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
Maliasili kumwaga neema ya ajira -MWANANCHI.

Tuesday, 21 August 2012 21:34


Mwandishi Wetu, Arumeru
WIZARA ya Maliasili na Utalii, inatarajia kuajiri jumla ya maofisa misitu 1000 Mwaka wa Fedha 2012/13 ili kupunguza tatizo la uhaba wa maofisa hao hapa nchini na hivyo kukabiliana na vitendo vya uharibifu wa mazingira.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alitangaza neema hiyo, katika mahafali ya 72 ya Chuo cha Misitu Olmotonyi kilichopo wilayani Arumeru mkoa wa Arusha.

Nyalandu alisema tatizo la ajira kwa maofisa Misitu, sasa litabaki kuwa historia hasa baada ya Serikali kuunda wakala wa misitu, ambao hadi sasa ikama yao inahitaji jumla ya wafanyakazi 2500.

“Serikali inathamini sana taaluma ya maofisa misitu kwani ni muhimu sana katika suala zima la utunzwaji na uhifadhi wa misitu nchini, ili kulinda Tanzania isiwe jangwa, ajira za maofisa misitu zilikuwa zimesimamishwa sambamba na ajira nyingine na serikali, lakini sasa zimerejeshwa”alisema Nyalandu.

Alisema kwa sasa hekta 90,000 za misitu ya uoto wa asili zinapotea kila mwaka kutokana na ujangili wa misitu,biashara ya kuchoma mkaa na kuvunwa bila ya utaratibu.

“Hivyo ili kukabiliana na changamoto hizi, serikali inahitaji kuwa na maofisa misitu wa kutosha na tuta waajiri wahitimu wote 121 wa mwaka huu katika chuo hiki,pia tutawahitaji wahitimu 107 wa mwaka jana na hata 101 wa mwaka juzi, wengine waliokuwa hawana ajira “alisema Nyalandu.

Akizungumzia matatizo ya chuo hicho, Naibu Waziri alisema wizara hiyo, itajitahidi kuyafanyia kazi, ikiwepo kurekebisha mfumo wa uongozi na hivyo kukipa fursa ya kujiendesha na kuweza kuajiri walimu.

Hata hivyo aliwataka wahitimu hao, kutumia taaluma hiyo vyema na kulisaidia taifa lao kukabiliana na changamoto za kimazingira na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho katika soko la ajira.


 
hawa jamaa ni sound tu mwana, wana zaidi ya miaka mitatu hawajaajiri, mbona hajasema ni tarehe au mwezi wa ngapi ajira zitatoka?. Halafu wanadai kuwa wana plan ya kuajiri Maafisa misitu 2,500 wakati idadi ya maafisa misitu ukiwajumlisha Tz yote hawafiki 1500. Ina maana asingealikwa ktk hiyo sherehe asingesema hiyo habari ya ajira au?
 
Back
Top Bottom