Misingi ya kujiajiri na kusimama kwenye miradi yako pasipo kutetereka

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Kujiajiri ni pale mtu anakua na wazo na kuamua kulifanyia kazi ili aweze kuongeza kipato chake yeye bnafsi bila kuambiwa au kusukumwa na mtu yeyote.

Kujiajiri Kuna husiana na kufanya shughuri ya ujasiriamali bila kupewa na mtu uifanye ni wewe unaanza kufanya ukiona inaleta faida.


Kujiajiri ni jambo linalohitaji maandalizi ya muda mrefu na kuna mambo ya msingi kuyafahamu ili kuongeza ufanisi ndo maana tunasoma ujasiriamali...

Namna ya kujiajiri

Tengeneza wazo rahisi linalo weza kutekelezeka kirahisi.....
Kama unataka kuwa mjasiliamali ni vyema ukawa umechagua eneo moja maalumu la kulitafutia ufumbuzi na ambalo rahisi kutekelezeka na pia kuwa makini na hilo jambo unalotaka kulifanyia kazi uwe na uzoefu nalo au Elimu japo hata kidogo, kwani huwezi kutibu ugonjwa usiojua hata unakaa wapi
Tambua jamii inahitaji nini kama unataka kuwa mjasiriamali ni lazima uwe na uwezo wa kuchemsha akili yako (UBUNIFU) katika kuyasoma mazingira uliyopo yanahitaji kitu gani na wewe ili uje na utatuzi wake. Lenga eneo moja ambalo unaona kweli lina uhitaji na unaweza ukaja na utatuzi wake..

Tengeneza lengo.

Kutengeneza lengo la biashara ni hatua muhimu katika hatua za kuwa mjasiriamali..... Lengo hili uliweke katika maandishi na litakusaidia katika kuwashawishi watu kukusaidia mtaji. Mara utakapokuwa umeandika lengo usikae bila kutafuta Namna ya kulitimiza

Hudhuria semina
Wewe kama unataka kuwa mjasiriamali ni lazima utenge muda wako kuhudhuria semina mbali mbali, zinazohusiana na shughuli unazotaka kuja kufanya au unazofanya.....


Jiunge na wajasiriamali

Ikiwa unataka kuwa mjasiliamali ni muhimu kutafuta eneo ambalo wajasiriamali wengi wanakutana kujadiliana,Katika mazingira kama haya utakuwa kama yai linaloatamiwa na kuku ili lije kutoa kifaranga kwa kupata mawazo chanya kwao.

Fanyia kazi hatari unayoifahamu
Sifa ya mjasiriamali wa kweli, ni yule asiyeingia kichwa kichwa kutaka kutatua tatizo pasipo kupiga hesabu za kutosha za hatari iliyopo. Mjasiriamali, kweli huwa anachukua hatari za jamii na kujibebesha yeye lengo kujifunza ili kubolesha.

Nidhamu

Kujiajiri ni ujasiriamali unaohusu faida, ukiwa mtumiaji rafu wa mapato huwezi kukua mpaka ufikie unapohitaji, na utaona kazi ngumu mno inatakiwa utulivu katika kutumia rasilimali wezeshe kwa faida ili usikate tamaa.

Nidhamu ni msingi katika ukuaji wa ujasiriamali.
 
Kuna kijana nilimsikia akisema mipango bila pesa ni makeleke.

Siyo tu kelele ni makelele!

Hata hivyo, utapataje pesa au mtaji bila kupanga ambayo ni sawa na kuwa na wazo au maarifa ya kupata mtaji na kuusimia?

Nami naona shida ya kwanza siyo mtaji. Maana wapo walio pewa mitaji na bado haikuwa ni suluhu.
 
Kuna kijana nilimsikia akisema mipango bila pesa ni makeleke.

Siyo tu kelele ni makelele!

Hata hivyo, utapataje pesa au mtaji bila kupanga ambayo ni sawa na kuwa na wazo au maarifa ya kupata mtaji na kuusimia?

Nami naona shida ya kwanza siyo mtaji. Maana wapo walio pewa mitaji na bado haikuwa ni suluhu.
Pesa itakuwezesha kupata hayo maarifa mfano kununua vitabu, kuhudhuria semina, bando, nauli za hapa na pale n.k
 
Back
Top Bottom