Misingi ya Azimio la Arusha, Falsafa ya Kujitegemea na Serikali ya Awamu ya Tano

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
* MISINGI YA AZIMIO LA ARUSHA, FALSAFA YA KUJITEGEMEA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO..

Awali ya yote, naomba niweke wazi ya kwamba, kwa hakika haiwezekani Azimio la Arusha la mwaka 1967, miaka sita tu baada ya Uhuru likawa ni lile lile miaka hii ya 2016. Litahitaji mabadiliko ili liende na wakati. Lakini ni ukweli pia ulio wazi, kwamba yapo mambo mengi ya msingi sana ambayo hayawezi kubadilika, ni ya faida kwa Taifa. Hayo ni pamoja na maadili kwa viongozi na msingi wa KUJITEGEMEA

Kuna baadhi ya wachambuzi au wanazuoni ambao ni wa mrengo wa uliberali, kwa makusudi au kwa kuujua ukweli wanaendelea na wataendelea kubeza misingi mikuu ndani ya Azimio la Arusha. Ili niweze kujenga hoja yangu vyema uchambuzi wangu kwa leo, utazungumzia msingi wa Taifa kujitegemea "Ndani ya Azimio la Arusha"

Kwa takriban miaka 30 (sio kipindi cha Mwalimu) ni jambo lililozoeleka kuona bajeti ya Taifa ina mchango wa wahisani kwa zaidi ya asilimia 43~50% ya fedha za maendeleo. Na kama haitoshi tumewahi kuwasikia viongozi wa kitaifa wakilalamika kuwa misaada haikufika kwa wakati na hivyo kushindwa kufikia malengo..

Ni jambo la faraja ndani ya miezi miwili ya Rais Magufuli (November na December) makusanjo yamekuwa kwa average ya 1.4 (November 1.3, na December 1.5). Hii ina maana kwa mwaka zaidi ya Trillioni 16 fedha za ndani zitakuwa zimepatikana (If trend will continue). Hivyo kwa bajeti ya kawaida kutakuwa na upungufu trillioni 4.2 tu.. Ambayo naamini serikali inaweza kutafuta vyanzo vingine na kupata hizo fedha... Na kama kutatokea ongezeko la Triilion mbili katika bajeti ya mwaka mpya, basi tutahitaji msaada mdogo sana na serikali itakuwa na fedha za ndani kwa zaidi ya asilimia 94.29%.

Naamini wote tunakubaliana kwamba ni katika kujitegemea ndipo maendeleo endelevu na ya kweli upatikana. Tunapokea fedha nyingi sana kutoka nje lakini bado hatujaweza kutoka kwenye mtego wa kupambana na maadui watatu, Ujinga, Maradhi na Umasikini. Ukweli ni kwamba fedha hizo na miradi mingi ya maendeleo inayoletwa na wageni hua na agenda za siri na mbaya zaidi hutufanya tuendelee kuwa tegemezi.

Ni vyema serikali hii ya Magufuli ikaweka mifumo ya kujitegemea. Mifumo hiyo inaweza kuwa ya kisheria au ya kisera. Japo yawezekana katika ulimwengu wa sasa wa ubebari uliokomaa na utandawazi uliotamalaki tunaweza tusifanikiwe kwa asilimia kubwa, ila ni muhimu kufanya uthubutu ili kuweka misingi imara ya vizazi vya mbeleni... Kwangu Mimi yafuatayo ni ya msingi katika hatua hii, ingawa mjadala ni mpana kwa wote...

1. Serikali ya awamu ya tano kuongeza makusanya ya mapato: Na lazima tukiri kwamba ndani ya miezi miwili trend imeonyesha average ya 1.4, hivyo pamoja na kuipongeza serikali, pia tutaiomba wazidishe juhudi na kukusanya zaidi ya hapo. La pili, ni kuwapa wito kwamba takwimu hizo zisibaki tu kwenye makaratasi, bali hudumu ziwafikie wananchi wa chini "economic perfomance ireflect poverty rate"

2. Ukomo wa Kupokea Misaada: Ni vyema tukaainisha wazi kwamba bajeti ya Taifa italazimika kuwa na asilimia ngapi kama fedha za ndani. Najua ukomo huo utaonekana kutunyima fursa ya kufurahia fedha za bure, lakini utatusaidia kuishi na kuendesha serikali yetu kadri uwezo wetu. Ukomo huu utatufanya kuwa makini katika kuchagua vipaumbele na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima

3. Ukomo wa Deni la Taifa: Sidhani kama nchi tuna kikomo/kiwango cha mwisho cha deni la Taifa (Ni kipindi cha Mwalimu pekee). Deni la Taifa ni kifungo cha kutojiamini, ni matokeo ya kutokuwa na maamuzi binafsi na ni aibu kwa taifa lenye utajiri kama Tanzania. Ukomo wa deni la taifa litalinda vizazi vyetu na kulipunguzia nchi na serikali zijazo mzigo. Mfano hii awamu ya tano imerithi mzigo mkubwa sana kutoka awamu ya nne

4. Marshati ya kupokea misaada ya Maendeleo: Kama taifa ni vyema tukajifunza kusema hapana kwa misaada iliyo na marshati magumu kwetu. Lazima tujue kwamba "principle" za ubebari ziko pale pale tokea enzi za ukoloni, na kinachobadilika ni "staructures" na agenda, hivyo misaada yao mingi inaambatana na unyonyaji ndani yake. Ni wepesi sana kutoa misaada pale agenda zao zinapopokelewa kwa shangwe. Ni jukumu letu kufanya uchambuzi wa aina ya misaada kwa kuangalia masharti yao..

Kwa mantiki hiyo, ni muda muafaka kwa watanzania chini ya usimamizi wa serikali ya awamu ya tano kurudia baadhi ya misingi mikuu ya Azimio la Arusha ambayo, mojawapo ni falsafa ya KUJITEGEMEA ili tuondokane na utegemezi uliokithiri. Nchi za South Asia walithubutu nao wakaweza (Kishore, 2010, Can Asian's Think). Kwa nini sisi pia tusifanikiwe?. Ni suala la mjadala wa pamoja!..

Mchambuzi Huru: Peter Kasera (BA Sociology, MA Development Management, Phd, on progress (DPAP)..
 
Back
Top Bottom