GE2025 Misime: Wanaotaka kuandamana waishie kuandamana hukohuko kwenye mitandao

GE2025 Misime: Wanaotaka kuandamana waishie kuandamana hukohuko kwenye mitandao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, akihojiwa na Kituo cha UTV, leo Jumanne Oktoba 14, 2025 amesema:

“Sheria ipo wazi wanaotaka kuandamana kinyume cha Sheria watachukuliwa hatua, Jeshi la Polisi tupo imara na tupo tayari kuwalinda Watanzania wema kwa nguvu tulizojaliwa na Mwenyezi Mungu pamoja na uwezo tuliowezeshwa na Serikali ya Awamu ya Sita.

“Watakaoandamana tutawashughulikia kwa mujibu wa sheria, kama kuna changamoto ichukuliwe hatua kwa mujibu wa Sheria.

“Watanzania wasiwe na hofu yoyote ile, Serikali yao imeliwezesha Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Usalama kusimamia usalama.”

“Wapiga kura wajitokeze kwa wingi kupiga kura wakimaliza warejee nyumbani, wasiwe na hofu, wanaosambaza hofu ni Wahalifu wa kwenye Mtandao, wanaeneza propaganda.

“Sisi tupo imara, pia ushirikiano tunaopata Jeshi la Polisi amani itatawala, watapiga kura na walioshinda watatangazwa.”
 
Sasa anahangaika nini kuzunguka kwenye mavyombo kama kuku anayetaka kutaga,si tukutane barabarani tu,kelele kama Mandonga
 
Back
Top Bottom