Mimi ninachofahamu ni kuwa hilo jopo la maulamaa wa kiislamu chanzo cha kuanzishwa kwake sio kujibu mapigo ya kanisa katoliki. Wazo la kuanzishwa jopo hilo lilitolewa pale Mzee Mwinyi alipopigwa kofi na kijana mmoja. Lengo la jopo hilo ni kutoa matamko mbalimbali (fatwa) kuhusu masuala mbali yanayowahusu waislamu, na kupunguza ile hali ya kila mtu kuamua kuwa msemaji wa waislamu.
Nathani hayo yanayojadiliwa hapa ni maoni ya mwenyekiti wa jopo hilo ambayo yamekuwa quoted out of context. Kwa utaratibu hayo majopo yana majina mbabalimbali mfano, Council of Scholars au Kule Irani wanaliita Guardian Council. Kwa kawaida rai ya jopo (fatwa) inatolewa kwa makubaliano ya wajumbe wote. Alichofanya mwenyekiti wa jopo hilo ni kutoa baadhi ya maeneo ambayo jopo linawaza kuyatolea tamko, na hiyo haiwezi kuwa ndio rai ya jopo kwani lilikuwa ndio linazinduliwa.