Mishahara ya watumishi wa umma sasa kupitishiwa CRDB badala ya NMB sababu ni nini hasa?

1. pole sana, kama ni kweli NMB ni wachivu hivyo kwanini CRDB hawajashinda kanda zingine TANO katika hizo SITA, na wakashinda MOJA tu.
Hawa ku bid kanda zote.
2. NMB MOBILE, mwanzilishi alikuwa ni CRDB, lakini aliingia cha KIKE kwani ilikuwa huwezi tumia bila INternet,NMb ndiye alikuja na JAVA capable aplication ambayo hata simu ya TOCHI iliweza kutoa Huduma.
Alisharekebisha. Microsoft analeta operating system kwanza sokoni na kufine tune bidhaa ikiwa sokoni, ndio principle ya fast services. Ukitaka kila kitu kiwe perfect hutaleta kitu sokoni. Angalia Boeing, Airbus, toyota nk
3. Swala la kutoa hela popote kwenye Mpesa, Airtel money kwa sasa hata Benki ya posta wanyo hiyo Huduma, NMB ni siku nyingi tu ipo. Wewe unazungumzia popote Tanzania, nbm hawana visa card, wenzao wanatoa sehemu yoyote duniani. Global village concept

4. Najua unajua ila uanjifanya hujuhi, Ukweli ni kuwa hakuna wa Kushindana na NMB kwa Idadi ya Matawi sasa yapo zaidi ya 200 nchi nzima, hakuna wa kushindana na NMB kwenye ATM kwa sasa zipo zaidi ya 500 nchi nzima, na atleast kila tawi lina ATM 2 hata NMB LITEMBO( naamini ndio tawi lilo porini kupita yote). Tenda ilikuwa ni ya kupitisha mishahara ya watumishi wa serikali kikanda, haikuwa kushindana nani mwenye matawi mengi. Stay focused.

5. Kinachotokea ni kuwa CRDB ni wajuvi wakupiga POROJo na PROMO, Pia kutoa RUSHWA, lakini kwa NMB ikiwa kama benki ya watu na wanahisa pia wanao iongoza wakiwa wazungu hawana muda wa kutoa rushwa na kupiga kelele, wao wanjiamini na huduma wanayio itoa na kama umeondoka wanajua utarudi tu, kama uamini nenda leo Tawi lolote la NMB na Chunguza kuna foleni ? na kama ipo chunguza ni ya watu wanao weka hela au kutoa?
Peleka TAKUKURU kama kuna ushahidi wa kutosha au PPRA vingenevyo hizo zitabaki kuwa ni hisia tu. Au unaweza kwenda CMSA, benki zote zipo list DSE kulalamika kuwa directors wao ni unethical.
 
Kweli bongo tuna sefari ndefu sana kufika world class company,,nina imani haitawezekana kampuni kutoka tanzania kufika level ya Samsung etc,,

Nimeshangaa sana NMB inajisifia ina matawi mengi sana eti yapo 200 (na hapo wateja anapewa kinguvu na serikali)

Juzi KFC wakati inafunguliwa outlet branch ya dar es salaam ilitangazwa ni branch yao ya 33,000 sijui na mia ngapi duniani ( na hapo hawabebwi na mtu wateja wanakuja kwa strategies).. Sisi kampuni zetu bado zipo kwenye 200,,

hivi toyota, sony, oracle, barclays ana branch ngapi duniani?

But tukiacha hayo yote NMB ana jitahidi sana maana hadi kijijini kwetu amefika..

Na wafanyakazi wake wana moyo sana maana kuna branch za NMB ziko porini mbaya lakini wapo wanapiga kazi kama kawaida
 
duh!mnatuletea waalimu huku crdb?

Yaaani hawa wapokea masihara kama watakuja na huku Crdb, kero za foren sasa kuwa Mount Everest. Acha nianze kufanya mazoezi ya kuvumilia harufu ya viatu na Vikwapa vilivyonikimbiza NMB.
 
Yaaani hawa wapokea masihara kama watakuja na huku Crdb, kero za foren sasa kuwa Mount Everest. Acha nianze kufanya mazoezi ya kuvumilia harufu ya viatu na Vikwapa vilivyonikimbiza NMB.

Ndugu acha dharau na majivuno.Kumbuka wewe ni binadamu kama hao wengine unaowadharau.Sisi binadamu we are nothing na kuna siku utakufa na kurudi mavunbini.Hata mitume kama Yesu walithamini na pia walikula na kunywa na watu masikini.Sasa jiulize wewe mwenzangu ni nani katika hii dunia?!

Dunia mapito ndugu na kila kiti utakiacha hapa hapa duniani!

Usimdharau binadamu mwenzako.

Pamoja na juhudi za kibinadamu, maisha mazuri ni majaliwa pia ya mwenyezi mungu.
 
Yaaani hawa wapokea masihara kama watakuja na huku Crdb, kero za foren sasa kuwa Mount Everest. Acha nianze kufanya mazoezi ya kuvumilia harufu ya viatu na Vikwapa vilivyonikimbiza NMB.
Kwanini usitumie zile card ambazo hela unaweza chukua kwenye ATM nyingi au nawe una hela za mawazo unaogopa makato,inaonekana nawe ni limbukeni tu huna lolote.Huwezi sema mwenzako ananuka kikwapa kwani chako hakinuki pengine ni zaidi
 
Huduma za kibenk CRDB ni mbovu kushinda NMB? Kwa kifupi CRDB imeshakuwa na wateja na portfolio kubwa kiasi kwamba haijali tena huduma, kila siku computer au system zake zinacrush kwa masaa, sasa upeleke utitiri wa account za watumishi wa umma si ni balaa? Hopeless!!
Mkuu usinikumbushe adha niliyopata jumamosi hii, nilijikuta nikifika mpaka jengo la ushirika Lumumba road kutokea Tawi la Kijitonyama, kila sehemu nikienda hakuna mtandao na mimi nilikuwa nahitaji pesa.

Kwa kweli kwa Benki hii usitumie mpaka ziishe kabisa nenda ukiwa na japo akiba ya kutumia siku hiyo kama ikitokea ukakumbana na adha ya kukosekana kwa mawasiliano.
 
duh!mnatuletea waalimu huku crdb?

Acha dharau wewe cashier a.k.a Bomba la kupitisha pesa kwenda kwa wenye pesa, wewe unabaki kusikilizia hurufu tu. Ina maana ualimu sio kazi, kama sio hao walimu hiyo keyboard ungegusa kweli ?
 
Yaaani hawa wapokea masihara kama watakuja na huku Crdb, kero za foren sasa kuwa Mount Everest. Acha nianze kufanya mazoezi ya kuvumilia harufu ya viatu na Vikwapa vilivyonikimbiza NMB.
Sio vizuri kudharau mtu mwingine kwa minajili ya kipato chake, huwezi jua mlala hoi wa leo ndiyo tajiri wa kesho na wewe tajiri wa leo ukawa mlala hoi wa kesho.

Siku zote walio nazo hawana makele na majivuno kama yako, jaribu kujifunza kuishi na ulimwengu vizuri na Mungu atakubariki.
 
Yaaani hawa wapokea masihara kama watakuja na huku Crdb, kero za foren sasa kuwa Mount Everest. Acha nianze kufanya mazoezi ya kuvumilia harufu ya viatu na Vikwapa vilivyonikimbiza NMB.

Acha dharau kwa watumishi wewe, ina maana pesa ya kuuza bangi ndio inakupa kiburi hivyo, kama wewe ni mjanja kwa nini usiwe na card ya umoja, waweza chukua pesa kwnye ATM zaidi ya tano. Aidha, kwa nini usitumie simu banking, unavuta pesa kutoka kwenye account yako ya benk, inaikuja kwenye acount ya simu, unaenda kwa Wakala wa Mtandao kulinga na simu yako unachukua pesa mahali popote bila jasho. Khaaa, kuwasema wenzio, kumbe bado wewe unaishi maisha ya miaka ya 80 !!!!
 
Kila hatua ya kuhama huwa tunapigwa trilion afu tunaongezewa kwenye deni la Taifa. Hata kutoka kwenye noti za zamani tulipigwa kitu hadi ATM zikawa zinatema fake Money. Hapa pia tutalizwa tuuuu!!!!
Kamati ya fedha/budget umkadidhi Andrew Chenge? Lini na lini, Fisi alinde bucha?
 
nilichoandika ni uhalisia na ukweli...yaani walimu ni noma iwe bank au ile ya zamani ya dirishani kwa mkurugenzi.
Mimi nasubiri wahamie crdb nirudi nmb,kamwe siliwezi timbwilitimbwili la walimu mwisho wa mwezi.

Walimu hawafai hata kama ndio waliotusomesha madarasani.Wengi wao wanakuwa kama hawajasoma wanashindwa kabisa kutumia ATM zile.CRDB is the best though they have few workers.
 
Kwan:(ini usitumie zile card ambazo hela unaweza chukua kwenye ATM nyingi au nawe una hela za mawazo unaogopa makato,inaonekana nawe ni limbukeni tu huna lolote.Huwezi sema mwenzako ananuka kikwapa kwani chako hakinuki pengine ni zaidi

Nina a/c hata huko but napendezewa zaidi na huduma za CRDB, kufundishwa na walimu siyo kigezo cha kunfumba kuandika ya moyoni.
Walimu hasa wa serikali ni Ovyo saaaaaaNa
 
duh!mnatuletea waalimu huku crdb?

Hahahahaaaaaa...umenichekesha sana aisee (najua unawazia kale kamsululu ka foleni kanakokua kule kwenye ATM za NMB...ukiita ..mwalimuu!...woote wanageuka nyuma), lakini nao pia si ni wateja tu kama wengine!!
 
Hahahahaaaaaa...umenichekesha sana aisee (najua unawazia kale kamsululu ka foleni kanakokua kule kwenye ATM za NMB...ukiita ..mwalimuu!...woote wanageuka nyuma), lakini nao pia si ni wateja tu kama wengine!!

mbona walimu wapo crdb toka zamani!kuna mshkaji wangu ana mwaka wa 6 kazini yupo crdb.msikariri!!!
 
Back
Top Bottom