Mkuu ulichoongea ni ukweli mtupu.
Ukikaa ukawangalia walimu wanapoanza kuwafundisha wanafunzi wasiojua chochote kichwani zaidi ya kurikaruka kama ndama juu ya madawati na kupiga makelele kama vichaa halafu mwalimu anamfundisha ustarabu na kuujaza ubongo wa mwanafunzi elimu inayokuza kipaji chake na kumpa mambo mengi aliyokua hayafahamu hata kuyaota basi utagundua kuwa kumdharau mwalimu ni kiburi tu baada ya kufanikiwa kijanja kijanja.
Watumishi wote wa umma wanahitaji kuheshimiana na kuona kuwa kila mmoja ni sehemu ya kulijenga taifa kwa uzalendo wa kweli.
Hii sio nchi ya kijamaa,jusema hii nchi ni ya kijamaa huku wananchi wanaishi kibepari ni unafiki mkubwa. Na huo ndio uongo mnaoaminishwa na wanasiasa mnawapa kura mnaendelea kua masikini.
Ujamaa uliisha enzi za Mwalimu. Hii akili naona kama magufuri anayo,itampa shida na hatimae atashindwa au atajikuta anachukiwa na kila mtu,kuleta mambo ya kijamaa ya kupangiana bei katika nchi ya kibepari.
Uzalendo hauko kwenye mshahara tu, unaweza kua unalipwa mshahara mdogo na bado ukawa mwizi,wafanyakazi wa tra wanalipwa mshahara sawa na wafanyakazi wa serikali kuu,tofauti ni kidogo ila ni wezi kuliko kawaida,the same na wanaolipwa mishahara mikubwa.
Ndugu yangu unachobisha hakina tija kabisa.
Wewe unaona kuwa ni haki na ni sawa kwa mwalimu,polisi, na wafanyakazi wa halmashauri mwenye digrii moja au diploma kulipwa mshahara wa kiwango cha chini cha mfanyakazi mwenye kiwango cha form four aliyeko TRA au Bandari au Maliasili au Mbunge na kwingineko?
Eti kisa wote watakula rushwa tu!!!
TRA wanakula rushwa kwa sababu polisi hawana mishahara ya kuwatosha lakini polisi wangekuwa na mawe ya kuwatosha TRA na wafanyabiashara wanaoshirikiana nao wangeozea jela mana polisi kila ukwepaji wanaujua na wanawakamata lakini kwa sababu ya njaa wanaachia ili nao waweze kusomesha angalau watoto wao.
Na huu ni mkakati kabambe wa kuwanufaisha wakwepaji wa kodi na watoa rushwa.
Akishaachiwa kule bandarini ili akwepe kodi anaambiwa polisi hawana shinda wewe wape hela kidogo tu watakuachia kwani wana njaa na mishahara midogo.
Halikadhalika kwa walimu wanapelekewa mpaka watoto vichaa ambao wangepaswa kusoma shule maalumu lakini wanahangaika kupigizana nao kelele mpaka wanachanganyikiwa kisa serikali inajua kuwa hawa watafanya kazi tu mana vimishahara vyao ni vya kukopea chakula kila siku kwa mangi na hawana ziada.