Mishahara ya wabunge itathminiwe upya

Wewe ni mbunge wa jimbo gani?
 
You've made my day...a very sensitive comment.
 
Mimi naona ipunguzwe ya Walimu sababu hawana akili
Tatizo la kuishi kwa kuzoea chuki na husda...hao walimu unaweza kumudu angalau 5% ya majukumu yao?
Try to be a real man or woman.
 
hapo ndo mi hukumbuka msemo mmoja nlioupata sehemu ukisema "democracy is hypocracy".yaan demokrasia imejaa full unafki.ila ndo hivyo huenda tukaja kuwa na serikali inayowajali wananchi wake kwa hali ya juu.
 
Sense.
Bado nafasi tunayo,tatizo tunaowaongelea ndiyo wenye rungu la kuyafanya hayo kwa mujibu wa katiba ya JMT 1977.
Kwa hiyo, ni ngumu kwa wabunge/mbunge kupeleka hoja binafsi ya kutaka punguzo la mishahara yao au sitting allowance zao.
 
Kwani hili bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria bila ya kubadili katiba? Trump kapangua mfumo mzima wa kodi wa Marekani juzi kwa kutumia kura za wabunge, sisi tunashindwa vipi.
Hatuna wabunge wa namna hiyo. May be over our dead bodies.
 
Million nane ingekuwa inalipwa kwa wabunge wenye akili timamu, wala hapana tatizo.

Kodi za wananchi zinatafunwa na hawa goigoi ngumbaru wasiolewa hata dhima yao ya kuwa ndani ya lile jengo.

Bunge thabiti linahitaji watu thabiti, sio hawa akili nyepesi.

Huyo msukuma hata ukimwambia maana ya subsidiary legislation anaelewa kitu gani pale?

Yupo tu pale kupiga soga na kucheka cheka hovyo!
 
Wanasiasa wetu ni tofauti sana na wanavyojiaminisha mbele ya umma.
Kwa hili la mishahara na marupurupu yao ni untouchable. Na hayatakaa yaguswe.Nafikiri hata Mh Rais akithubutu kutumia mamlaka yake katika hili,ajiandae kujiongezea maadui na wengi wao kutoka chama chake.
Nafikiri kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu mabadiliko ya katiba.Bado tunaihitaji katiba ya Warioba.Vinginevyo, tumekwisha na hatuna pa kutokea.
MP's are selfish...hawatokwi povu kwa maslahi ya umma, bali kwa maslahi yao tu.
 
Hii Nchi Pengo kati ya mwenyenacho na asiyenacho ni kubwaa mno, na kwa Muono wangu pengo hilo linazidi kukuwa siku hadi siku, kama suala hilo litaachwa bila mkakati wowote wa kupunguza pengo hilo basi Taifa kwa ujumla hatutakuwa salama. Bwana Jean-Jacques Rousseau aliwahi kusema, Nanukuu " When the poor shall have Nothing more to Eat, they will eat the Rich" Mwisho wa kunukuu.
 
Inshallah....Rais wetu msikivu ataifanyia kazi hoja hii.
 
Katika mambo haya ya msingi wana mshikamano wa kutisha. Hutamsikia kubenea wala maji marefu.
 
... " When the poor shall have Nothing more to Eat, they will eat the Rich" Mwisho wa kunukuu.
Capt John Komba alipata matatizo na gari lake manzese akashangaa vijana wa pale badala ya kumsaidia, walipora baadhi ya vitu. Wengine tukasema ingeshangaza kama asingeporwa. Ni hali isiyoepukika.
 
Capt John Komba alipata matatizo na gari lake manzese akashangaa vijana wa pale badala ya kumsaidia, walipora baadhi ya vitu. Wengine tukasema ingeshangaza kama asingeporwa. Ni hali isiyoepukika.


Ukiangalia kiuhalisia Makabwela tuko wengi kuliko mabwenyenye, kwaiyo mambo kama hayo hayawezi kuepukika
 
Ubunge iwe ni kazi ya kujitolea,ila wapewe posho stahiki wakati wa vikao vya bunge
Sifa ya mbunge iwe Mtanzania mwenye uwezo wa kujitegemea sio wasaka malupulupu kupitia ubunge.
Kama ilivyo kwa madiwani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…