KERO Responded Mishahara ya ‘Staff’ wa DAWASA Kibaha inatoka wapi kama zaidi ya Miezi MITATU Bili ya Maji ni Unit 0!

KERO Responded Mishahara ya ‘Staff’ wa DAWASA Kibaha inatoka wapi kama zaidi ya Miezi MITATU Bili ya Maji ni Unit 0!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
354
Reaction score
1,039
Mimi ni Mkazi wa Maili Moja, Kibaha Mkoani Pwani, huku kwetu Mtaa wa Muheza na mitaa mingine ya jirani kwa takribani zaidi ya miezi mitatu sasa tunapata bili ya maji Unit 0 ikiwa na maana hakuna maji kabisa.

Wakati sisi tunahaha na kusota kwa kukosa huduma muhimu ya maji kwa muda wote huo najiuliza Serikali inawalipaje mishahara Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji yaani DAWASA Kibaha kama hawaingizi kitu chochote kwa muda wote huo!

Ndio maana taasisi na kampuni nyingi binafsi zinapiga hatua kimaendeleo tofauti na zile za Serikali kwa mambo kama haya, Bosi hawezi kuendelea kumlipa mtu ambaye haingizi faida kwa miezi yote hiyo, unakuwa na faida gani sasa?

Hawa Mabosi wa DAWASA Kibaha tena ukute wanajilipa na posho ya vikao, fedha inatoka wapi? Waziri wa Maji naye yupo kimya wakati hii kero ipo muda mrefu na kelele zinapigwa kila siku, tukiwauliza Viongozi wa DAWASA Kibaha hawana majibu ya kueleweka.

Kuna Injinia mmoja wamempa kazi ya kuwa anafuatilia huduma ya maji huku kwetu lakini hatoi ushirikiano kabisa na anakuwa mkali pindi tukiuliza kwa nini hatuna maji kwa kipindi chote hiki.

Tunajiuliza hao mabosi wa DAWASA Kibaha na kwao hakuna maji kama sisi, au ndio wanashirikiana na watu wa madoza kuwauzia maji? Maana pale kwenye ofisi zao dumu moja ni sh 3,000 kisha wao wanakuja kutuuzia huku dumu moja Shilingi 30,000 hadi 35,000!

Majibu ya Mamlaka ya Maji ~ DAWASA: Kweli Muheza – Kibaha kuna shida ya maji, tunasubiri Mradi wa Pangani, kuna mpango wa kuchimba kisima
 
Huyo uliemtaja hapo analipwa au halipwi?
 
Wanarudisha Maendeleo Nyuma. Yaani Kuanzia Uliowataja. Wote ni walewale huku kwetu tumeng'oa mabomba
 
yaani hisi chuo chaji kinazaliwa wataalamu wenye maji vichwani
 
Back
Top Bottom