Mishahara ya Polisi ya mwezi wa pili

Mishahara ya Polisi ya mwezi wa pili

MUSIGAJI

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2014
Posts
2,261
Reaction score
2,741
Wakuu poleni na majukumu!

Kuna jamaa mmoja tunaishi naye mtaani hapa ni askari polisi.Tarehe 2 mwezi wa pili aliomba nimkopeshe fedha kiasi na akaniambia angeirejesha mapema maana wanalipwa mshahara katikati ya mwezi na mwisho wa mwezi.

Ilipofika katikati ya mwezi nikaona kimya nami nikapiga kimya,Mwisho wa mwexi umefika nikaona kimya jana nikaamua kumuuliza akasema bado mishahara yao ya mwezi wapili haijaingia.Naomba kuuliza kwa wanaojua ni kweli haijaingia au tayari maaskari wameshapata mishahara?

Assnteni wakuu
 
huyo hataki tu kukulipa deni lako mshahara toka trh 25 mfukoni
 
Ila hata mimi nilizipata tetesi za kucheleweshewa mishahara yao ya mwezi wa pili yaweza kuwa ni kweli.
 
Hawa nao wana hakika lakini norkim 1991 kaongezea yake

Ndio maana ya kuwa na jukwaa mgongano wa mawazo
 
Wakuu poleni na majukumu!

Kuna jamaa mmoja tunaishi naye mtaani hapa ni askari polisi.Tarehe 2 mwezi wa pili aliomba nimkopeshe fedha kiasi na akaniambia angeirejesha mapema maana wanalipwa mshahara katikati ya mwezi na mwisho wa mwezi.

Ilipofika katikati ya mwezi nikaona kimya nami nikapiga kimya,Mwisho wa mwexi umefika nikaona kimya jana nikaamua kumuuliza akasema bado mishahara yao ya mwezi wapili haijaingia.Naomba kuuliza kwa wanaojua ni kweli haijaingia au tayari maaskari wameshapata mishahara?

Assnteni wakuu

imeingia juzi.
 
Swala la kukopa na mshaara linahusiana nn? Tambua mshaara ni siri ya mfanyakazi na mwajiri tu sio vinginevyo, Mwambie akulipe hela yako aache ujanja ujanja..kwani shida haina mwisho
 
Kuwa mvumilivu kama utaona kimya mbaka tarehe kumi mfuate nina hakika awezi kuwa na kisingizio kingine.
 
yaani hawa wasipewe kabisa hiyo mishahara na ukome kuwakopesha wanyama hela
kopesha watu.
 
Hana nia ya kukulipa huyo. Mshahara tumeshakula hadi tunaufikiria wa mwezi Machi.
 
Usimkopeshe wala kumpangisha nyumba polisi. Itakula kwako. Mwisho utazushiwa kesi!
 
Back
Top Bottom