Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,661
- 119,284
Wanabodi,
Rais Magufuli Akizungumzia Mishahara ya Peponi.
Kwenye tamko la Rais Magufuli, kuhusu watu kulipwa mishahara minono kama ya peponi, alitoa tuhuma nzito ya posibility za bodi za mashirika hayo, kuhongwa na menejiment ili ku collude kuipitisha mishahara hiyo!. Na kwa vile mashirika hayo ni umma, baada ya bodi hizo kuhongwa ndipo wakaiptisha mishahara hiyo, kabla haijaanza kulipwa, mawaziri husika waliliarifu baaza la mawaziri kuhusu mishahara hiyo!. Kama bodi zilihongwa, zikapitisha, then kuna uwezekano hata hao mawazii nao walihongwa na kuleta cabinet na kuitetea, ila jee pia kuna uwezekano wa mkuu wa cabinet naye alihongwa kuipitisha?!. Hili ni swali lenye kuhitaji tafakui ya kina!.
Bado nalitafakari kwa makini, tamko hili la rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, kuhusiana na mishahara mikubwa, kumbe kuna uwezekano bodi za wakurugenzi, wa mashirikia yaliyopitisha hiyo mishahara mikubwa zilihongwa?!. Wenyeviti wa bodi, ni wateule wa rais, na maamuzi ya bodi, lazima yaungwe mkono na serikali kupitia wizara husika, hivyo kama tuhuma hizi za rais Magufuli kuwa kuna uwezekano wa bodi hizi kuhongwa, kunamaanisha pia kuna uwezekano, mawaziri na makatibu wakuu wa wizara zenye mashirika ya wanaolipwa mishahara minono nao pia walihongwa, ndio maana wakaridhia viwango hivyo?!.
Maamuzi ya mawaziri, hupelekwa katika vikao vya baraza la mawaziri kupitia cabinet paper za wizara husika!, ambazo huwasilishwa na waziri husika na kutetea hoja zake!, ambapo mkuu wa kikao hiki ni rais wa nchi, sasa kama ni kweli, kuna uwezekano, wakuu wa bodi walihongwa kupitisha mishahara minono, mawaziri nao wakahongwa kupitisha viwango hivyo hadi kuja kwenye cabinet, jee hakuna uwezekano kuwa huyu mkuu wa cabinet naye alihongwa ili kuridhia viwango hivyo?!.
Nawaombeni wanabodi msije kunipaura as if ni mimi ndio niliousema huu uwezekano wa kuhongwa, aliyeusema uwezekano huo ni rais wetu mchapakazi Dr. John Pombe Magufuli, msikilize kwa makini kwenye hiyo video clip, niliyoinyofoa kwa yule jamaa yangu!.
Kama ni kweli kuna uwezekano huo wa menejmenti za mashirika wanaolipa vizuri, walihonga bodi ili kupitisha mishahara hiyo minene, na wenyeviti wa bodi hizo ambao ni wateule wa rais, walihongwa wakawasilisha viwango hivyo vya mishahaa kwa mawaziri husika, inamaanisha huo uwezekano wa kufanya maamuzi kwa shinikizo la hongo, pia uwezekano huo, unaweza ukawahusu mawaziri hao kuhongwa, ili kuwasilisha viwango hivyo kwenye kikao cha Cabinet, na kama ni kweli walihongwa ndio wakafanya hivyo, then, pia kuna uwezekano wa cabnet nayo yote ilihongwa, akiwemo mkuu wa cabnet ili kuridhia viwango hivyo?!.
Kuna kanuni inasema uongo ukisemwa na kuachwa bila kukanushwa, maana yake ule ni ama ni kweli ni uongo tuu, ila kutokana na kutokukanushwa, then unageuka ndio ukweli, au zile hisia kuwa watu walihongwa sio hisia za uongo bali ndio ukweli wenyewe!, na kwenye kitu kinachoitwa "admissibility of guilty", "silence means guilty!".
Tangu rais Magufuli alipotoa tuhuma hizi za posibility za bodi za mashirika hayo kuhongwa, sijabahatika kumsikia hata mwenyekiti mmoja wa bodi yoyote ya haya mashirika ya mishahara minene, akikanusha bodi yake kuhongwa, ili kupitisha viwango hivyo, then tulitegemea wenyeviti wa bodi hizi waliopo, angalau wajitokeze kunawa mikono, kuhusu tuhuma hizi kwa bodi zao kuhongwa, kwa kueleza bayana kuwa wao walipoteuliwa kuongoza bodi hizo, walikuta tayari viwango hivyo vya mishahara menene vimepitishwa na bodi zilizotangulia kabla yao, hivyo kama kweli kuna hoja kuhongwa, then waliohongwa sio hao waliopota sasa, bali ni wale, ni wenyeviti wa bodi zilizopitisha hiyo mishahara ya peponi!.
Kwa maoni yangu, tamko hili la rais linahitaji kuzingatiwa kwa makini sana na hata ikibidi litolewe ufafanuzi, mimi kwa masikio yangu, nimemsikia rais akisema atahakikisha hakuna Mtanzania analipwa zaidi ya milioni 15!. Hakusema kuhusu watumishi wa umma wala hakuzungumzia taasisi za umma, amesema Watanzania!. Unless mniaminishe, kuwa rais wa nchi anapowazungumzia Watumishi, anamaanisha ni watumishi wa umma pekee ambao yeye ndio mkuu wao!.
Namalizia kwa kukumbusha swali la msingi, kuwa kama issue ya Mishahara Minono ya Peponi!, Bodi Zilihongwa!, then kuna posibility pia Wawaziri Nao Walihongwa ili kuwasilisha mishahara hiyo cabinet, swali linabaki jee cabinet nayo ilihongwa kupitisha?!, jee mkuu wa cabnet, ambaye ni Rais Jee, naye kunauwezekano Alihongwa?!, nijuavyo mimi Ikulu ni mahali patakatifu, hakuna uwezekano wowote kwa rais wa nchi kuhongwa!, jee Magufuli alipozungumzia uwezekano wa bodi hizi kuhongwa, alimaanisha bodi tuu, lakini sio wale waliopitisha viwango hivyo na kuridhia vitumike?!.
Nawatakia Jumatano Njema.
Pasco.