Tuchukue kwenye group ya TGS kwenye wizara,kiongozi mkuu ni Katibu mkuu,hivyo ukiona maximum salary jua ni mshahara wa katibu mkuu.
kwa hiyo iko hivi.Kuanzia juu kabisa.
TGHS L
TGHS L (Sh 3,400,000) - Katibu Mkuu wa Wizara
TGHS K
TGHS K (Sh 3,100,000) - Mkurugenzi/Kamishna/Mkuu wa idara flani hapo wizarani
TGHS J
TGHS J (Sh 2,900,000)- Mkurugenzi Msaidizi/Kamishna Msaidizi/Mkuu wa kitengo flani ndani ya Idara
Endelea kushuka chini kwa kuangalia Hierarchy ya ukubwa hapo wizarani kwenu.
sasa kwa hawa mabwana hii mishahara ni 20-30% ya mapato yao ya mwezi,kwani wana vikao lukuki wanavyolipwa,wana stahili za kila mwezi,wana allowance zisizoisha,hivyo usishangae Mkurugenzi kuwa na total income ya 8-10M kwa mwezi.na vyote hivi ni haki zao za msingo,kabla ya kuanza kufisadi sasa.kwa wale mafishadi hiyo 10M ni weekly change.kwa mafisadi papa hata mshahara huwa hawachungulii!