Mishahara makatibu wakuu wa CCM, Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mishahara makatibu wakuu wa CCM, Chadema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mlengo wa Kati, May 14, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Malumbano kati ya viongozi wa CCM na Chadema yamendelea kupamba moto, safari hii Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akitangaza hadharani mshahara aliodai ni wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, kwa madai ya kutaka kuthibitisha kuwa halipwi fedha nyingi.
  Kauli ya Nape aliyoitoa jana ni juhudi za kutaka kuusadikisha umma kwamba mshahara wa bosi wake haufui dafu kwa mshahara wa Katibu Mkuu wa (Chadema), Dk. Willbroad Slaa.
  Nape alisema kuwa Mukama analipwa mshahara wa Sh. milioni 1.5 na posho ya mwezi ya Sh. 300,000.
  Juzi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Chadema, Mabere Marando, alisema Mukama analipwa mshahara wa Sh. milioni 11 wakati Dk. Slaa analipwa Sh. milioni 7.1, hivyo CCM hawana sababu ya kushangaa mshahara wa Slaa.
  Malumbano hayo ya mishahara ya viongozi wa vyama hivyo viwili yanatokana na kauli ya Nape kuwa Dk. Slaa ameshinikiza kulipwa mshahara mnono akieleza msimamo huo unakinzana na wakati akiwa mbunge alipokuwa akishinikiza malipo kwa wabunge yapunguzwe.
  Nape alidai kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni sawa na wa mbunge.
  Hata hivyo, uchunguzi huru wa NIPASHE uliofanywa juu ya mishahara ya viongozi watendaji wa CCM umebaini kuwa makatibu wa CCM wa mikoa wanalipwa mishahara ya Sh. milioni moja baada ya kodi, wakati makatibu wa wilaya wanalipwa Sh. 700,000 baada ya kodi, ilahali Katibu wa UVCCM akitia kibindoni Sh. milioni 1.5.
  Kwa vigezo vya mishahara hiyo, ni sawa na kusema kwamba mishahara ya makatibu wa jumuiya na pengine ya makatibu wa mikoa haitofautiani na ile ya katibu mkuu.
  Vile vile jana, Nape amekanusha madai yaliyotolewa na Mwanasheria wa Chadema, Marando kwamba yeye (Nape), alikwenda kuomba agombee ubunge Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya chama hicho na wakamkatalia kwa kukosa sifa.
  Akizungumza na NIPASHE jana akiwa mkoani Singida, Nape alisema Chadema ndio walimfuata na kumwomba achague jimbo la kugombea kupitia chama hicho.
  “Waliniambia nichague Jimbo lolote la uchaguzi Dar es Salaam nigombee isipokuwa Ubungo, lakini nikawakatalia, niliwaeleza wazi kuwa mimi kuhama CCM ni sawa na kumsilimisha Papa sasa hiyo kauli ya Marando ni uzushi wa hali ya juu,” alisema Nape.
  Alidai hata alipohudhuria Baraza Kuu la chama hicho walimuomba avae sare za chama hicho na kisha kumwomba ajiunge na chama hicho, lakini alikataa na hata sare alizijaribu na kuwarudishia hapo hapo.
  “CCM ni chama kikubwa na kinapata ruzuku kubwa kuliko Chadema, lakini angalia mshahara wa Katibu Mkuu wetu linganisha na Sh. milioni 7.5 anazolipwa Dk. Slaa, Marando ameamua kwa makusudi kuupotosha umma hivyo kama ni muungwana basi aombe radhi kwa Watanzania aliowadanganya,” alisema Nape. Alisema mshahara wa Mukama unalipiwa kodi wakati wa Dk. Slaa haukatwi kodi hivyo alimshauri kwanza kujisalimisha kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kulipa kodi anayodaiwa.
  “Kutolipa kodi ni ufisadi wa hali ya juu, lakini mtu huyu huyu ambaye halipi kodi anajifanya ana uchungu na umaskini wa Watanzania, hata pale ofisini kwake kuna watu wanalipwa mishahara midogo hata haitoshi kujikimu kwa siku kumi, kuna msemo kwamba kabla hujatoa boriti kwenye jicho la mwenzako anza kutoa kwako,” alisema Nape.
  “Tafsiri ya fisadi kwa mujibu wa Ilani yao ni mtu anayeishi kiujanja ujanja, sasa Dk. Slaa anaishi kwa mtindo huo maana huwezi kukwepa kodi inayotumiwa na serikali kuwaletea maisha bora wananchi, kisha mtu huyo huyo ukajifanya unawapenda Watanzania,” alisisitiza.
  Alisema hata Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alifanya ufisadi kwa kukiuzia chama magari makuu kuu aina ya Mitsubishi Fuso, ambayo chama kilikuwa kimeyakodisha kwa ajili ya matumizi yake.
  Kuhusu madai kuwa alinufaika na fedha za EPA, Nape alisema huko ni kutapatapa kwani hawajawahi kutajwa katika kashfa hiyo tangu ianze miaka mingi iliyopita na wameanza kumpakazia baada ya kuanza kuwashambulia.
  “Hivi siku zote wanawataja wahusika wa EPA kwanini wasinitaje na mimi, leo hii wameona nimeanza kuanika maovu yao ndipo wanaanza kuhangaika kutafuta mambo ya kutunga, waambie Chadema ukivuliwa taulo chutama usikimbie, walizoea kusema wenzao sasa yamewageuka wanahaha” alisema.
  Kuhusu madai kuwa anapokea mishahara miwili, wa U-DC na wa CCM, Nape alisema alishakabidhi ofisi hiyo siku nyingi na madai hayo si ya kweli kwani hajawahi kupokea hata mshahara mmoja tangu ateuliwe katikati ya mwezi uliopita.
  “Tangu niteuliwe sijapata hata mshahara mmoja, inamaana Marando anamaanisha kuwa nalipwa mshahara kila wiki,” alihoji Nape.
  Alisema gari analotumia hivi sasa ni mali ya CCM tofauti na madai ya Marando kuwa anatumia gari la serikali.
  Juzi Marando akiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho, Anthony Komu, waliwaambia waandishi wa habari kuwa mashambulizi ya Nape dhidi ya chama hicho yanatokana na chuki na hasira aliyonayo baada ya kukataliwa kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam.
  Kadhalika, chama hicho kilidai kuwa mshahara wa Sh. milioni 7.1 anaolipwa Dk. Slaa na chama hicho ni kiasi kidogo ikilinganishwa na ule wa Mukama wa Sh. milioni 11.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Pimeni wenyewe? Mtu huwa na asira sana akiguswa huo nadhani ni mwanzo tu. Slaa ajue yeye ni mwana wa kitatange umma un imani naye lakini kwa hili anatusaliti hasa ukizingatia kima cha chini ni 135,000 mpaka 7,100,000 si mchezo kwani cdm siyo ccm? Ni wapiganaji wa wanyonge, au ni ile kauli ya baba kushiba kwanza ili akawatafutiee watoto? Aangalie madiwani wake tabu wanazopata, wananchi wanavyotabika, hivyo yeye hastahili kuishi nyumba ya vioo kama kiongozi wa ccm anayegombana naye kila siku
   
 3. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nape anafuata nyayo za tambwe hiza. Bravo j. Makamba, unaweza kuokoa jahaz la chama chako, lakn kwanza watoe akina nape na wenzake, hawakisaidii chama chenu.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Binafsi napata shida sana kusoma hizi habari za Nape na mshahara wa Dr Slaa kwa sababu sioni tija yake kwa Taifa. Nape anaweza kuueleza umma ccm na serikali yake wana mkakati gani kuhakikisha failure rate ya form IV mwaka huu inabadilika? Au ana updates kuhusu mgao wa umeme? Na ajira je, ile hadithi ya 1m imefikia wapi? Anavyoonekana huyu Nape ni kama mtu mchunguzi mchunguzi which is good maana anaweza kutuambia sisi wananchi serakali inakopa misharaka kwenye bank za biashara au la? Hivi ndio vitu nilitarajia vimtoe Nape ofisini kwenda kwa wananchi na sio majungu ya kupakana matope.

  Lakini yeye anashupalia mshahara wa mtu mmoja mmoja kama sera wakati anashindwa hata kuweka bayana malipo (sijatumia neno mshahara) ya either yeye binafsi au katibu Mukama. Baada ya mis-steps za 90 days za kujivua magamba nilifikiri Nape angekuwa amejifunza na kuwa makini zaidi juu ya nini cha kusema. Juzi alinukuliwa akimtaja Dr Slaa kwa kutanguliza neno Padri huku akitaja mambo binafsi ya Slaa sasa leo anakuja na mshahara wa Slaa.very trivial things.

  Sasa hivi hana njia, aandae notes zenye mashiko ili zimsaidie wakati chadema watakapotoa (in details) malipo ya timu yake Nape. Umbea sio sera.
   
 5. General mex

  General mex Senior Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Thenki yu so machi, tunataka sera zitakazobadili sura ya nchi hii na sio kuulizana mishahara.
   
 6. I

  Iso Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Wanasiasa walete sela za kuikomboa nchi kutoka kwenye umasikini.kuliko kutajiana mishahara haisaidii chochote.
   
 7. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  MTU MZIMA NGUO ZIKIMVUKA HUCHUTAMA. ukiona ni kinyume na hapo ujue huyo si mtu mzima bali ni umbo tu. NAPE NA CCM malipo anayopata DR SLAA hayakuwekeni ninyi ktk usafi kwa kashfa nzito za ufisadi zinazoendela na kuangamiza maisha ya walio wengi, kiimsingi haziwasaidii Wananchi kuondokana na hali hiyo, KENYA viongozi wanaanza kujadili ni vipi wapunguze gharama za maisha zinazopanda kila kukicha, UGANDA juzi rais baada ya kuampishwa (baada ya mbinyo toka kwa wapinzani) ametoa mikakati yake ya kupambana na hali hiyo. Ninyi hapa mnapeana ruzuku uzunguke nchi nzima kumzungumzia mtu binafsi , hivi bado mnafikiri kuwa WATANZANIA HAWA NDIO WALE ALIOWATAWALA NYERERE....?
   
 8. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  ...Nape Nnauyeee.. Unatuaibisha wana Mzumbe!!
   
Loading...