Mishahara hewa: Mkurugenzi Utumishi wa Umma asimamishwa

Qualcomm

Senior Member
Nov 27, 2013
177
138
Kutokana na kukithiri kwa malalamiko kuhusu mishahara na kukithiri kwa tatizo la mishahara hewa serikali imesitisha mkataba wa ajira ya Emmanuel Jerome Mlay, Mkurugenzi wa Idara ya USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU KATIKA UTUMISHI WA UMMA, idara inayoshughulikia mishahara ya watumishi katika utumishi wa umma.

Uamuzi huu umefikiwa Katika kuimarisha utendaji na ufanisi wa idara inayoshughulikia mishahara katika utumishi wa umma.

Bwana Mlay yuko katika likizo inayoishia tarehe 30 April 2016, siku ambayo ajira yake inakoma.
 
Kutokana na kukithiri kwa malalamiko kuhusu mishahara na kukithiri kwa tatizo la mishahara hewa serikali imesitisha mkataba wa ajira ya Emmanuel Jerome Mlay, Mkurugenzi wa Idara ya USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU KATIKA UTUMISHI WA UMMA, idara inayoshughulikia mishahara ya watumishi katika utumishi wa umma.Uamuzi huu umefikiwa Katika kuimarisha utendaji na ufanisi wa idara inayoshughulikia mishahara katika utumishi wa umma. Bwana Mlay yuko katika likizo inayoishia tarehe 30 April 2016, siku ambayo ajira yake inakoma.
Sidhani kama unaweza kumwachisha kazi / kumpa notisi akiwa likizo; kinachopaswa ni kukatiza likizo yake na kumkabidhi barua ya kukatiza mkataba wake na salio la likizo litakuwa sehemu ya malipo yake
 
Mkurugenzi wa Utumishi yeye angefanya nini.Tatizo hilo limeanzia kwenye maafisa utumishi wa halmashauri na taasisi za serikali.Mfumo wa ajira na utumishi,ulipaji wa mishahara haupo sawa.

Mkuu huna haja ya kuwatetea. Hawa ndio wacheza deal wakubwa. Wale maafisa utumishi wa Halmashauri kazi yao nikuwaletea deal wizara ya utumishi. Utumishi ndiye Mwajiri mkuu. Kwa hiyo bila kumshirikisha huyu hao wa Halmashauri hawawezi kufanikisha mpango wao. Madeal haya hufanywa pia kwa kuwashirikisha maafisa kutoka Hazina. Kumbuka ili pesa ya mshahara wa mtu yoyote itoke, lazima Hazina wa liason na utumishi kuhakikisha kuwa huyo mtumishi ana exist. Yaani Wizara ya utumishi ikisimamia hili kwa makini hakutakuwa na mtumishi hewa hata mmoja
 
Mkurugenzi wa Utumishi yeye angefanya nini.Tatizo hilo limeanzia kwenye maafisa utumishi wa halmashauri na taasisi za serikali.Mfumo wa ajira na utumishi,ulipaji wa mishahara haupo sawa.
Huyu mara nyingine analetewa stop order yeye hafuti,repoti za CAG zinatoa majina hewa miaka na miaka yeye hafanyii kazi.
 
Sidhani kama unaweza kumwachisha kazi / kumpa notisi akiwa likizo; kinachopaswa ni kukatiza likizo yake na kumkabidhi barua ya kukatiza mkataba wake na salio la likizo litakuwa sehemu ya malipo yake
Wewe nae sio mzima.kwenu ukiwa likizo auko kazini.au ujawahi kuajiriwa !!? .sii ukija kazini unakutana na barua yako.
 
Mwaka huu watumishi wote watafukuzwa. Kwenye idara na wizara zote za serikali, watumishi wote watakuwa wapya. Awe mwangalifu asije jifukuza na mwenyewe.
Mwaka huu kila hatua itakayo chukuliwa mtalia tuu maana tumesha gundua hamko sawa vichwani!
 
Back
Top Bottom