Una uhakika hujalewa?Misemo mingine ilitungwa na Wahenga waliotoka kunywa Pombe na katika zama hizi za haifai kuendelea kutumika kwani inafanya jamii iamini ujinga kuwa ni busara na hekima.
Una uhakika hujalewa?
... kajifunze maana ya fasihi hususan methali na tamathali za semi Mkuu.
Hahahahahaa we jamaa bwana,yani na unajiona umeandika kitu maikini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]...okey hata huo mfano uliotolea unamaana kifasihi.Tamathali za semi ni lazima ziwe "conceivable".---- inatakiwa ziendane na hali halisi ya tungo mama.
Hivi kiuhalisia, wewe unaweza kumpa mchawi amlee mwanao??!, mchawi ni shetani iweje umkabidhi ili amlee??.
Hii inaweza kusababisha watu wengine nao walete tungo zao mfano; "Ukitaka kujua ubaya wa dhambi mfuate shetani". ---je tamathali kama hiyo inaingia akilini???.
Tafakari.
Mmeona tatizo lenu.Yan unaamini wadada wanavaa nguo za wazi ili kuonesha nyuchi zao ili wazae?ni upungufu wa akili kuamini hivi."Mficha uchi hazai" hii methali imesababisha dada zetu kuvaa nguo za ajabu ajabu ilimradi wasiwe wagumba.
Kwann mchawi?
Kwasababu kwa hofu ya kuwa wanamjua yeye mchawi,hawezi kumdhuru maana jamii inajua akipata matatizo tu basi yeye ndo muhusika.kwa kujua hilo mchawi hatomgusa huyo mtoto kwa ubaya kwa kuogopa vidole vya jamii.
... asante Mkuu kwa ufafanuzi murua! Pia ni muhimu kuelewa kwamba wakati mwingine fasihi hutumia lugha ya kinyume ili kutimiza lengo kusudiwa iwe ni kufunza, kuonya, kuadabisha, n.k. Ni sawa na mzazi anamkabidhi kijana wake ada ya shule huku akimwambia "chukua hii ada ukaile tena kama ulivyokula ile nyingine"; sasa hapa Ndugu Mokaze angetuambia mzazi amemruhusu mwanae akale ada! Hataki kushirikisha ubongo ajue maana ya mzazi ni kuonya na sio kuruhusu.Hahahahahaa we jamaa bwana,yani na unajiona umeandika kitu maikini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]...okey hata huo mfano uliotolea unamaana kifasihi.
Ni kweli huwezi kujua ubaya wa kutenda mabaya kwa kumfata mtu ambaye hatendi mabaya.kwa lugha nyepesi ukitaka kuujua ubaya wa wizi mfate mwizi,siku atakapokamatwa na kupigwa mawe ndipo utakapojua kuwa wizi una ubaya huu.
Shetani ametumika kama mtu ambae ni mtenda maovu,anaweza kuwa yeyote ie mwizi,malaya,nk.
... tatizo wanachukua maana mzobemzobe jinsi inavyosomeka au kutamkwa bila kushirikisha ubongo! Tatizo la msingi liko hapo Mkuu.Mmeona tatizo lenu.Yan unaamini wadada wanavaa nguo za wazi ili kuonesha nyuchi zao ili wazae?ni upungufu wa akili kuamini hivi.
Jiulize kufucha uchi kwa namna gani?
Mbona wanaume wanaonesha nyuchi zao na hawazai?
Mbona malaya wanaoonesha nyuzi zao kwa watu wengi sio hao wenye watoto wengi mitaani?
Jibu ni moja,ukitaka matokeo unayoyahitaji,lazima vitendo viendane na uhitaji wa matokeo hayo.
Mwanamke atamaniye kupata mtoto,ni lazima uchi wake auoneshe(wasex) ili apate mtoto.
Unaumwa na unatamani kupona,lakin hutaki kudhihirisha ugonjwa wako kwa daktari,unategemea kupona vip?nro hapa tunasema mficha magonjwa kifo humuumbua,maana umeshindwa kuonesha ugonjwa ili upone
Kabla hujaandika huu uzi ulitakiwa uwaulize Waswahili wanaitumiaje misemo hii. Uzi wako uneonyesha ni kwa namna gani hukijui unacho kiandika na hili ni tatizo kubwa. Mathalani msemo wa kwanza ulio unukuu, huwezi ukamkuta Mswahili anautumia bila kuzingatia muktadha wa hali,, muktadha wa hali ambao akiutumia msemo huo unaleta maana ya wazi kabisa, huo msemo wa pili, ndio daaah, uko wazi na kuwatahadharisha watu juu ya kutenda haki hata kwa mtu mnyonge wa namna gani,bali mpaka kwa mtu unaye mchukia.Ni mambo ya kushangaza kuona watu na akili na busara zetu bado tunashikilia misemo isiyokuwa na maana bali kupotosha jamii, eti utasikia ikisemwa; "Mpe mchawi alee mwanao" au utasikia; "Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake".
Mchawi ni mtu mbaya sasa iweje umpe mwanao amlee?!--- je akimfundisha uchawi au akimlisha nyama za watu utamlaumu nani??-- kama neno mchawi ni tamathali kwanini tamathali hiyo inathibishwa na kitu kibaya?
Pia utasikia Mnyonge mnyongeni lakini apewe haki yake, sasa mtu kisha nyongwa (kawa marehemu) ni kwa vipi atapewa haki yake?--- au atapenyezewa akiwa kaburini?
Misemo mingine ilitungwa na Wahenga waliotoka kunywa Pombe na katika zama hizi za haifai kuendelea kutumika kwani inafanya jamii iamini ujinga kuwa ni busara na hekima.
Kuna mtu nimeona kajaribu kukudadavulia.Kama na hapo hujaelewa basi acha kufuatilia methali kabisa."Mambo ya kumpa mwanangu mchawi amlee"??!!🤣
Kama ukubwa ndio akili za aina hiyo basi naomba nisikue.