Inconvenient Truths
JF-Expert Member
- Oct 21, 2014
- 439
- 354
Yes
Desperate times call for desperate measures. Hakuna production kwa sababu serikali iliopo madarakani inapiga vita private sector. Wachahe waliopo makazini wameachishwa kazi na wengine wamepunguzwa. Sasa serikali imeamua msaada wowote ule utakaokuwa unapelekwa kusaidia masikini na kupunguza ukali wa maisha utatozwa Kodi pamoja na VAT
Maana yake ni kuwa; misaada ya vitabu kwa mashule, madawati, visima vya maji, nguo, vifaa vya mahospitalini, vitu vya kuwasaidia Maalbino na wasiojiweza vyote hivyo vitatozwa kodi.
Mfano, unaleta kontena la futi 40 la vifaa vya shule kwenda kusaidia shule au hospitali Morogoro au Tukuyu au Mkuranga au Nyarugusu, na haya kama tayari una barua zote toka kwa walengwa, mkuu wa wilaya, mbunge, mkuu wa mkoa etc kuthibitisha hayo bas jua utalipishwa Kodi kamavile umeleta vifaa vya biashara na ukishindwa bas jua kontena litapigwa mnada na TPA na TRA kwa sababu serikali ina hali ngumu sana ya kifedha hivyo haioni taabu kuchukua vya maskini na wasiojiweza kwenye jamii
Habari ndio hiyo.
Zidumu fikra za mwenyekiti....!
ushauri. Kama unapenda sana kusaidia hao maskini bora peleka kwenye nchi ambazo wako tayari kupokea hiyo misaada pasipo kutozwa kodi na usithibutu kupitisha Kontena hilo la transit Bandari ya Dar kwa sababu utapigwa VAT
Maana tusharudi kwenye Dar Ages