wa hapahapa
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 7,460
- 4,402
Zinatumika kwenye nini Sasa?
Ambulance kwa mkoa wa dar...
Zinatumika kwenye nini Sasa?
Sio kweliUtashangaaa fedha hizi zinakwenda kujenga reli
Wamlipe mkandarasi wa flyover ya ubungo amalize kazi haraka,tunataka kuwahi kuchapa kazi,foleni zinazingua
MISAADA ya kusaidia Serikali kukabiliana na janga la corona imeendelea kumiminika na kufikia zaidi ya Sh. bilioni 6.726, ikiwa ni fedha taslimu na vifaa. Jana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokea hundi ya mfano ya Sh. milioni 500 kutoka kampuni ya Export Trading Group (ETG) kwa ajili ya kukabiliana na janga hilo linaloitafuna dunia.
Waziri Mkuu alipokea msaada huo jana ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma, kutoka kwa Mkurugenzi mkazi wa ETG, Nilladri Chowdhury. Wiki iliyopita Waziri Mkuu, pia alipokea zaidi ya Sh. milioni 6.226 kutoka kwa wadau mbalimbali nchini, kwa ajili ya maji tiba na barakoa za kuwasaidia wananchi na watumishi wa afya katika kukabiliana na janga hilo.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Waziri Mkuu aliwashukuru watendaji wa kampuni ya ETG kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya virusi vya corona, ambapo hadi sasa kesi 49 zimeripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huo nchini na wagonjwa saba wameshapona. Aliwataka wananchi wote wazidishe kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo hasa katika kipindi hiki.
“Hatua tuliyofikia hivi sasa, maambukizi yameanza kuongezeka hasa kwa Dar es Salaam na Zanzibar. Tunajua kule kuna watu wengi na shughuli zote za kiuchumi zinaanzia pale, lakini hatunabudi kufuata masharti tuliyopewa ili kuzuia ugonjwa huu usisambae,” alisema. “Serikali inatoa msisitizo kwa wananchi wazingatie maelekezo yanayotolewa kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona ikiwamo kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka pamoja na kujiepusha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.” “Muhimu zaidi sote tuendelee kumuomba Mwenyezi Mkungu ili atupunguzie makali ya ugonjwa huu,” alisisitiza.
Awali, Mwenyekiti wa Kampuni ya ETG, Mahesh Patel, Mkurugenzi Mkazi wa ETG, Nilladri Chowdhury, alisema wameamua kuchangia ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika vita ya kupambana na ugonjwa huo.
Alisema kampuni yao inashughulika na masuala ya kilimo ikiwamo kusambaza pembejeo na kuongeza thamani mazao kupitia kampuni yao ya Kapunga iliyoko Mbeya, viwanda vitatu vya kubangua korosho vilivyoko Mtwara, Newala na Tunduru na viwanda vya kusindika mbegu za mafuta.
Pia, wanatoa soko kwa wakulima kwa kununua mazao kama korosho, mbaazi, kokoa, mahindi, choroko na ufuta. Corona ilianzia kwenye mji wa Wuhan China, mwishoni mwa Disemba mwaka jana, na kwa mujibu wa kituo cha utafiti cha Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani, hadi jana jumla ya watu 1,934,583 wanaugua ugonjwa huo.
Aidha, watu 120,863 wameshafariki na nchi au maeneo ya utawala yenye maambukizi ni 185, huku nchi iliyoathirika zaidi ni Marekani yenye watu 582,634 wanaougua na kati yake 23,649 wamefariki.
CHANZO: Nipashe
Misaada ya shs.6.2 nakumbuka ilikuwa tarehe 8 April, kulikoni tena!

Utashangaaa fedha hizi zinakwenda kujenga reli
Tutamalizia kuleta zile ndege! Na hizi fedha za emergency sidhani kama zinakuaga audited. CCM wamepatia za Uchaguzi humo humo ndio maana hawakua serious kukemea hilo Gonjwa kumbe wametegaUtashangaaa fedha hizi zinakwenda kujenga reli
Tuwasiliane inbox
Au atapewa Polepole akanunue madiwani wa upinzani
Ina maana hakuna watu wanaojitolea kwa ajili ya taifa lao ndo kutukuamini tu kwamba inwezekana.Vice versa is true wanaotoa unawajua?? Kwa awamu hii kupenda sifa haiachi kumpa mtu pesa akaenda kuweka japo tu ionekane inaungwa mkono.

.