chumachakavu
Member
- Oct 1, 2017
- 55
- 103
Jamani hii sio fair!
Watu maarufu ndiyo wakilia shida kidogo wanasaidiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi sisi kajamba nani hakuna kitu kama hicho.
Kwa wale wafutiliaji wa kipindi cha njia panda cha Clouds na kile cha ushauri wako cha RFA mtakuwa mashahidi. Watu wanashindwa kupatiwa matibabu kwa kukosa laki 5 na wanasema wamepita kwa viongozi kadhaa nao wanawaambia nendeni redioni.
Hata baada ya kueleza shida zao redioni hutasikia kiongozi fulani amesaidia, ila ikiwa maarufu kama Jetman, Wastara, Sajuki utasaidiwa kwa asilimia mia ufe kwa mipango ya mungu ila sio fedha.
Viongozi wetu mbadilike, saidieni na wasio maarufu kwa nguvu ile ile, sio sisi kajamba nani mnatusaidia magongo ya kutembelea halafu mamilioni kumi na mnawasaidia watu maarufu.