Misaada inaweza kuingizwa Syria katika maeneo manne ya mipaka

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,103
Katika takribani miaka sita iliyopita Umoja wa Mataifa na makundi mengine ya misaada ya kiutu, umefanikiwa kuvuka mpaka kuingia Syria kutokea Uturuki, Iraq na Jordan, ikiwa ni maeneo manne ambayo yameidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupeleka misaada ya kiutu kwa mamilioni ya watu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amsema mataifa 15 wanachama wa baraza hilo, yanalengo la kuongeza muda wa operesheni hiyo wiki hii. Hata hivyo Urusi imetaka kupunguzwaa kwa idadi ya maeneo hayo ya vivuko.

Azimio lililoridhiwa na Ubeligiji, Kuwait na Ujerumani lilipendekeza kuongezwa kwa maeneo ya vivuko vya mipakani vya kuingia Syria taifa lililochakazwa na vita na kufikia vitano kwa kukijumuisha cha tatu cha Uturuki, lakini Urusi ilipinga kwa kusema itakubali viwili tu kwa upande wa taifa hilo.
 
Back
Top Bottom