Mirathi itanitoa roho, naombeni ushauri la kufanya

Mirathi itanitoa roho, naombeni ushauri la kufanya

Pole sana dada kwa kufiwa na mume ungali bado mbichi. Mungu atakutangulia na kukupa mwongozo juu ya kulea wanao.

Kuhusu mirathi fuata ushauri wa wadau hapo juu.
 
nenda TWLA watakusaidia, hiki ni chama cha wananasheria wanawake, haki yako iko wazi
 
Habari wana Jukwaa.Mimi ni mwanamke wa umri wa miaka 32.nilifiwa na mme wangu sasa ni miezi sita toka afariki.
Alifia hapa DSM na kuzikwa kijijini kwao huko mkoa flani sitaki kuutaja jina kwa kuhofia usalama wangu.
Aliumwa nikauguza na akanifia mie mwenyewe.Tumejenga Nyumba moja na tuna shamba.Tulifunga ndoa ya kanisani.

Tatizo linakuja kwenye kufungua mirathi ya mme wangu.Maana alikuwa mtumishi wa serikalini.
Shemeji zangu wanataka mirathi tufungulie kijijini kwao.na mie nataka tufungulie hapa DSM maana ndipo tunapoishi na kujenga tumejenga hapa na kufia kafia hapa pia cheti cha kifo kinaonesha kafia hapa DSM.

Hawa shemeji zangu hawana nia njema na mie maana tayari wameshaanza chokochoko za kutaka kunitoa kwenye nyumba niliyojenga na marehemu mme wangu.Kwa kisingizio ipangishwe ili watoto wapate ada ya shule.
Tulifanikiwa kukaa kikao cha kuteua misimamizi wa mirathi mwaka jana Dec na wakaniteua mie nikisaidiwa na shemeji yangu.ila kwa ugomvi mkubwa sana walitaka wao wawe wasimamizi.
Mwisho wasiku tukaafikiana na wao kazikatalia zile karatasi za kuteua msimamizi wa mirathi wakazipeleka weyewe mahakamani bila mimi kunishirikisha.Hakimu akawarudisha akaaambia waje adi mie niwepo.

Basi wapendwa naomba msaada kwa yeyote anae jua wapi nianzie ili niweze kufanikisha kufungua mirathi huku hata kama ni shirika au taasisi yeyote inayoweza kunisimamia kwa hilo.

Tatizo dogo hilo sister. Waone LHRC

Legal And Human Rights Centre

con_address.png
Justice Lugakingira House
Kijitonyama
P.O. Box 75254 Dar Es Salaam Tanzania

con_tel.png
+255 22 2773038

con_fax.png
+255 22 2773037

twitter.png
@http://www.twitter.com/humanrightstz

facebook.png
http://www.facebook.com/humanrightstz

website.png
http://www.humanrights.or.tz

























Justice Lugakingira House
Kijitonyama
P.O. Box 75254
Dar Es Salaam, Tanzania
+255 22 2773038
http://www.humanrights.or.tz



 
Asanteni sana wapendwa.Naanza kazi hiyo wiki ijayo ntatembelea kote huko LHRC TAWLA TAMWA zote ntazitembelea na nitachukua likizo ya wiki nzima adi ni settle hii mambo.Jasho langu haliwezi kwenda bure.
 
Pole kwa msiba, very simple tafuta wakili lakini pamoja na hayo usikate tamaa maana is not a simple road. So far uko kwenye sehemu nzuri.
 
Pole sana dada,
Miezi sita tu ndugu roho ziko juu juu.

Wanapoteza tu muda na pesa lakini mwisho wa siku kila kitu
kitakuwa ni chako.

Fuata ushauri unaopewa hapa.
 
Mi hua nashangaa sana...hivi inakuwaje mali atafute mtu mwingine alafu wewe uzitolee macho....Kwa nini usipiganie cha kwako...hadi kuanza kumnyang'anya mjane.

Dada...wewe komaa...ikiwezekana nenda LHRC watakusaidia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom