Miradi ya Ujenzi inayoendelea Chato inahitaji mjadala wa kitaifa

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
12,499
50,988
Duka la MSD tayari limefunguliwa chato wakati halipo Katoro wala Geita...

Uwanja Wa ndege unaendelea kujengwa Wa kiwango cha kimataifa pale chato..

Shule ya kisasa kama fadhila pale rais aliposomea ingawa hii siwezi pingana nayo shule ni muhimu.....

Hayo yote hayashangazi lakini kituko ni jengo la TRA lenye gorofa linajengwa Chato ...

Kwa wafanya biashara wapi?
Kwa uchumi upi?

Katoro kwenye biashara TRA wameshindwa kujenga jengo la kisasa?...

Kichekesho ni kuwa kampuni inayojenga vitu hivi vyote ni moja wala hakuna cha tenda kutangazwa ....

Hivi hii nchi watu wote ni vipofu kweli ..

Unawezaje kujenga jengo la billion 10 halafu wilaya haina uwezo Wa kukisanya hata bilioni 2 Kwa mwaka ...

Mapato ya chato mwaka Jana kwenye halimashauri yalikuwa milioni 300 yaani hata hayajitoshelezi kujiendesha mpaka waombe serikali kuu....

Je Hawa TRA watatoa wapi pesa za kukusanya ?....

Kiukweli project zinazoendelea chato inabidi zianzishe mjadala Wa kitaifa.....

Tuambiwe kuna faida gani kuwa na jengo la TRA lenye thamani ya billions of money chato lakini si katoro kwenye biashara?...

Hivi chato kuna nini awamu hii why always Chato?

Jengo la TRA chato linalojengwa Kwa kasi ya ajabu sijui wataenda kukusanya kodi maporini......
56458c2f2501438620ee06d1a3b15082.jpg

9E749853-9493-4DCB-A6A0-8E8DBED0AA56.jpeg


Ukweli lazima usemwe hata kama unauma



MASWALI YA TUNDU LISSU:
Jana Mhe.Tundu Lissu aliuliza maswali manne ya msingi kuhusu shughuli mbalimbali zinazoendelea wilayani Chato, na mimi naomba kuyarudia hapa kama ifuatavyo:

1. Kwanini uwanja wa ndege mkubwa (International Airport) unajengwa Chato wakati makao makuu ya mkoa wa Geita hayana hata uwanja wa baiskeli? Kwanini pesa za kujenga uwanja wa Chato ambako ni wilayani zisingetumika kujenga uwanja wa ndege makao makuu ya mkoa huo?

2. Kwanini kuna taa za barabarani katika Kijiji cha Chato wakati hazipo katika miji yote jirani kama Geita, Kahama, Bukoba, Kigoma, n.k? Unawekaje taa za barabarani kijijini (Chato) halafu makao makuu ya mkoa na miji jirani hayana taa hizo?

3. Kwanini ofisi ya TRA yenye ghorofa mbili inajengwa Chato wakati wilaya hiyo haina mapato yoyote ya maana ukilinganisha na miji jirani kama Katoro, Geita au Runzewe? Kwanini ofisi hizo za kisasa za TRA zisingwjengwa Geita mjini, Katoro au Runzewe?

4. Kwanini jengo kubwa la MSD linajengwa kijiji cha Chato wakati Makao Makuu ya Mkoa hakuna duka la MSD?

5. Kulikua na sababu gani za kufuta mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na kuanzisha ujenzi wa uwanja ndege Chato? Makosa yaliyosababisha mradi wa bandari ya Bagamoyo kufutwa, hayawezi kuwa hayohayo yaliyosababisha Airport ya Chato kujengwa?

Maswali haya aliuliza Mhe. Lissu jana
 
Duka la MSD tayari limefunguliwa chato wakati halipo Katoro wala Geita...
Kwahiy kumbe yalikuwa ni makubaliano ya wawili!!

Miezi kadhaa iliyopita, Ruangwa imefunguliwa ghala la MSD!! Kwa watu wasioifahamu Kusini, Ruangwa ni remote na imekuwa wilaya miaka michache tu iliyopita!

Remoteness ya Ruangwa inashindana na Liwale!! Lakini pamoja na yote hayo, MSD Ruangwa ndiyo inatakiwa kuhudumia mkoa wa Lindi na Mtwara... kwamba, mkoani wanatakiwa kufuata madawa wilayani ambako hata kufikika kwake wakati mwingine ni changamoto!!!

Binafsi kwa umaamuma wangu wakati ule nikahoji imekuaje Mkulu kamkubalia PM kufanya haya... kumbe it's a matter of time; kumbe ilikuwa ni quid pro quo deal... nipe nikupe!

Nipe International Airport na Medical Store nakupa Medical Store!!!

I love Tanzania!!!
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amezindua duka la dawa la MSD Wilayani Ruangwa

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amezindua duka la dawa la MSD Wilayani Ruangwa, lililopo ndani ya hospitali ya Wilaya hiyo na kuzusema kuwa hiyo ni hatua ya serikali ya kuboresha huduma ya afya kwa kuwawezesha wananchi kupata dawa kwa wakati na kwa bei nafuu.

Amesema duka hilo limewekwa wilayani Ruangwa kwasabu eneo hilo lipo katikati ya wilaya za Liwale, Kilwa na Nachingwea hivyo wananchi wa maeneo hayo na hata mikoa jirani watafaidika na huduma hiyo.
Kisha Medical Store Department wanaonesha mgawanyo unaotia shaka ya kule wapi kuna bohari zao!
Duka la Ruangwa linafanya maduka ya MSD mpaka sasa kufikia Sita, ikiwa ni pamoja na mengine yaliyopo Arusha, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam na Chato.
 
Una wivu wa Kike. Bahati nzuri ni kwamba hiyo yote si miradi ya Rais. Rais akimaliza muda wake bado wana Chato wataendelea kuitumia
Wewe ni kiboko, yaani kabla hata hujasoma tayari umeshajibu, ila mtoa mada anataka kujua hiyo bajeti imeidhinishwa na nani?. Na bunge au wizara ya Fedha?. Nchi lazima iendeshwe kwa Mujibu wa sheria tulizojiwekea wenyewe.
 
Una wivu wa Kike. Bahati nzuri ni kwamba hiyo yote si miradi ya Rais. Rais akimaliza muda wake bado wana Chato wataendelea kuitumia
Swali ni kuwa; kuna walipa kodi wepi chato kulinganisha na katoro!?? Uwanja wa ndege wasafiri wepi kulinganisha na Mwanza? Duka la MSD kwa sababu watu wa chato ni bora kuliko wa Katoro.
Chato iwe makao makuu ya wilaya au mkoa basi tujue moja!! Zimwi la ubinafsi limezidi hapa hata ukabila haufui dafu kwa sababu huu ni ufamilia/ukoo
 
Una wivu wa Kike. Bahati nzuri ni kwamba hiyo yote si miradi ya Rais. Rais akimaliza muda wake bado wana Chato wataendelea kuitumia
Hujajibu hoja umbaki na mipasho ya kichoko
Makusanyo ya halmashauri 300million TRA wanajenga kukusanya nini
Uwanja wa ndege wa kimataifa kwa kijiji cha watu 17000 wa nini?
Kwanini miradi inajengwa na mtu moja bila kutangazwa tenda
Usidhani tumesahau ya mv Dar es salaam
 
Katika nchi hii wajinga ni watu wa kusini tu, vile tumejazana serekalini tena ktk nafasi za juu, tena hakuna nafasi tusioshika katika nchi hii lakini bado kusini ni kubovo kupindukia. Hii ni aibu kweli
Butiama kwa Mwalimu (rip) kumekuja kuendelezwa alivyoacha urais.

huyu ndiye mfano wa kiongozi muadilifu. siyo hawa wengine na hao uliotaka eti nao (selfishly) waendeleze kwao!!
 
Back
Top Bottom