Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,712
- 41,468
Sote tunajua ile miradi ya kipuuzi iliyopigiwa sana chapuo na Bashe, aliyoiita ni miradi ya ajira kwa vijana.
Kupitia miradi hiyo, wizi mkubwa wa pesa umefanyika. Walisema kuwa gharama ya kuandaa ekari moja ni shilingi milioni 7.
Ile miradi ni upuuzi wa hali ya juu. Wanaotaka kupata uthibitisho, waende Nzega ambako kuna mradi wa wizi mkubwa wa pesa ya wananchi. Mradi huo pekee umegharimu mabilioni ya pesa kwa kuwapa kandarasi marafiki zake katika kuweka fence na kutengeneza barabara fake kuzunguka eneo lote, kujenga nyumba na kuweka mitambo ya umwagiliaji maji isiyomwagilia kwa sababu hakuna maji. Bwawa dogo la Kilimi ndiyo Bashe anawadanganyia watu kuwa eti ndiyo litatosheleza kumwagilia shamba lenye ukubwa wa ekari zaidi ya 1,000, wakati bwawa hilo ni dogo sana na wala haliwezi kuwa na maji ya kumwagikia hata ekari 100 wakati wa kiangazi. Bwawa hilo lilichimbwa miaka ya huko nyuma na lilitumika kama chanzo cha maji ya kutumia majumbani kwa wakazi wa Nzega. Hata kwa matumizi tu ya majumbani, maji hayo hayakuwa yanatosheleza wakazi wa Nzega.
Rais Samia ni wa kuonewa huruma, jinsi mawaziri wake wanavyomchezea, na yeye kukosa uwezo wa kupambanua mambo. Mwakajana Samia alipelekwa kwa mbwembwe kwenye shamba hilo akidanganywa kuwa litazalisha mbegu za mahindi za kutumika nchi nzima. Naye akaamini, na bango lipo pale likieleza shamba hilo la upigaji wa pesa ya umma limefunguliwa na Rais Samia.
Mmoja wa makandarasi, siku moja nikiongea naye, alikuwa akitamba kuwa kwenye hizo tenda, hawezi kunyimwa kwa sababu yeye akishalipwa huwa anawakumbuka.
Waandishi wa habari za uchunguzi, nendeni Nzega mkashuhudie lile shamba kichaa lililokula mabilioni ya pesa lakini hali ya mazao ni aheri mashamba ya wananzengo ambao hawajaenda shule hata darasa moja.
Pesa ya umma inachezewa na kufisadiwa na wakuu wa Serikali kwa kupitia miradi bandia ya kilimo. Hili la kusema kuwa eti ni miradi ya kuwasaidia vijana, ni dili kubwa la pesa lililotengenezwa na kusukwa kiujanja sana, na hatimaye wakafanikiwa kumchota Rais, naye bila kutafakari karuhusu watu waibe pesa ya umma.