Mgongo wa paka
JF-Expert Member
- Oct 3, 2011
- 485
- 36
Yanayotokea CUF na NCCR ni matunda ya dhambi ya usaliti ya vyama hivyo dhidi ya matakwa ya dhati ya wananchi wa Tanzania baya. CUF na NCCR vimekuwa siku zote vikicheza tune za CCM. Huu nauona kama ndio mwanzo wa mwisho wa vyama hivyo katika ulingo wa siasa za upinzani za bara. Vitabaki majina tu kama ilivyo Tadea, TLP na UDP.
Hata wewe huamini umesahau huwa unasema Zanzibar ni mwalimu wa siasa bara waje kujifunza huko.hawa watu wazima ni wajinga sana, sasa kujivua nguo mbele ya hadhara kunawasaidia nn ?
haya mambo nilishazoea kuyasikia kwa akina Wema na Diamond na wenzao
sikuamini ambao wanaaminika kama wanasiasa makini wanafanya mambo ya kijinga kama haya
Havina migogoro kwa sababu havina ruzuku, kama hutaki pressure jiunge na chama kisicho na mbunge.R I P ur self coz taasis mnayoiombea ife ina wabunge 32 sijui tukuelewe vp inapata ruzuku ya kutosha. Vipo vyama havina wabunge lakini havifi.
Jussa anadai Hamad ni mroho wa madaraka, mchuuzi anayemuonea gere urafiki wake na Rostam.
Jussa anadai Hamad ni kirusi asiyejua maadili ya uongozi kwa kuchukua nyaraka za chama na kuzi-publish kwenye kitabu chake.
Anaendelea kushusha tuhuma kwa Hamad kwamba alikuwa akiongoza wabunge kutokulipa fedha ndani ya chama kama katiba ya CUF inavyowataka kufanya hivyo kwa kulipa 10% ya mapato yao ya ubunge. Alikuwa akificha pay slip na Jussa alipoteuliwa kuwa mbunge na Kikwete miezi sita ya bunge lililopita aliwaumbua kwa kupeleka pay slip kwenye chama
akseh, mmenifungua macho, kweli haya sikuyajua juu ya upinzani wa kitanzania, eh mola tusimamie watanzania kwani hatuna mwenyewe, my sincere thanks and appreciation to jamii forum, with full of great thinkers. Duh asentiduuuuuh, sihasaaaaa, ukiona vinaelewa ujue vimeundwa na umdhaniaye ndiye siye, wazo langu: Tufute vyama vyote tuwe na kimoja tu kama china, labda huu upuuzi wa kudanganya wananchi walalahoi utaisha,
Alikuwa anaficha. Ayaongee kwani hayo ni mazuri? sasa hivi wamechanganyikiwa wameamua kuvuana nguo.Huyu Jussa alikuwa wapi siku zote asiyaseme hayo mambo yote?
Mmhhh, viongozi wa taasisi za kidini wako salama katika hili?
Watu mmesahau jameni. Suala hili la CUF kufadhiliwa na Rostam liliandikwa na Kulikoni na This Day, mwaka wa juzi kama sikosei. Ilielezwa kwa uzuri sana kuwa viongozi wa juu wa chama hicho walikuwa wakikutana kwa siri na Rostam katika kupeana ufadhili. Mwandishi mmoja wa habari ambaye kwa sasa yuko serikalini, aliwahi kuitwa na Rostam hoteli moja kubwa Dar es Salaam, kwa ajili ya kupanga mikakati fulani, kwa manufaa yao, akamkuta pale Chacha Zakayo Wangwe! Wakati huo jamaa ndiyo anaisumbua CHADEMA balaa, kila mkiambiwa anatumwa/kutumiwa huyo, yuko kwenye pay roll, watu hawaamini. Uongozi wa juu wa CHADEMA kwa umakini wao, walishamuona siku nyiiiiiiiiiiiingi, Chacha anavyotaka kuharibu course for change. Baada ya Chacha, nafikiri walitafuta mtu/watu wengine na wakafanikiwa. Lakini uzuri watu wote makini wanajua nani ni nani kwenye hii course.
Haya ni matokeo ya kuwa na vijana ambao ni too ambitious for money and power. Halafu unasikia wanapiga makelele nchi ikabidhiwe vijana, nchi ikabidhiwe vijana...waogo, walaghai, wanafiki, walafi wakubwa hawa wa madaraka na mali. Hatari! Na wote walioko katika mtandao wa akina Rostam na Lowassa, vijana waliogawanyika katika vyama mbalimbali, wanajuana, utawasikia katika vyombo vya habari na mijadala mbalimbali wanavyohusiana na kuteteana. Angalieni nyuma ya pazia. Ufisadi unapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote. Ndiyo maana CHADEMA kupitia kwa majemedari, Mbowe na Rais Slaa, wameliweka hili kuwa ni kipaumbele namna moja. Hate the game and the player(s) too. This is a syndicate brothers kuweni makini sana!
RA ndie alietoa oda kwa rais kumteua Jussa kuwa mbunge cunajua, rais na ra ndio wenye dowans
If that's true, sina maneno rahisi ya kuelezea zaidi ya "Mola wetu tuhurumie waja wako". Hivi huyu RA ni nani hasa kiasi cha kuifanya nchi yetu, viongozi wetu, na sisi wenyewe mateka kiasi hicho?
Si huyu huyu aliwahi kutuhumiwa kuingilia hadi uchaguzi wa viongozi wa kanisa fulani? Hii nchi iko hatarini kuliko tunavyodhani na zaidi ya wakati mwingine wowote katika historia yake!
Wameshatumika na ccm tayari, na sasa kazi yao ni kama imeisha..pandikiza migogoro kati yao ili kuondoa nguvu yao!
Ni kweli kabisa mkuu, tumekwenda na maji. Huyo RA akabidhiwe tuu hii nchi iwe inajulikana kuwa ni ya kwake na familia yake. Kila sehemu ni RA na karibu kila chama cha siasa ni RA, vyombo vya habari kama magazetini ni RA, makanisani ni RA. Mungu atunusuru kwa kweli.
Nilkuwa siamini wakisema RA ndio rais, huyu Jussa ubunge atakuwa aliteuliwa na swahiba wake RA kupitia JK.