Mipangilio ya expire date inavyochanganya

Mipangilio ya expire date inavyochanganya

Maguge Maguge

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2016
Posts
2,734
Reaction score
1,780
Expire date ya bidhaa ni kitu muhimu sana, lakini niseme, ni rahisi sana watu kutumia bidhaa zilizoharibika, na hata baadhi ya wauzaji wanaweza kuuza bidhaa zilizoisha muda wake kutokana na kushindwa kuchambua mikanganyiko iliyopo, ukizingatia kwamba wauzaji na wanunuzi ni watu wa hali ya kawaida.

1.Inaandikwa kwa kiingereza ingawa inakuwa bidhaa ya kuuza ndani ya nchi inayotumia kiswahili kama lugha ya Taifa

2. Ina mipangilio tofauti tofauti
Kiasi kwamba kwa mtu mwenye upeo wa kawaida ni vigumu sana kuchanganua

Mfano wa kwanza:
P:17.6.2016/F524
E:16.06.2019(a)bc

Wa pili:
19-09-04-17

Wa tatu:
LOT 23D MFG AUG 2015EXP AUG 2020
REG .NO.TAN 00,535 NO2BEH

Wa nne:
MFG MAY 2016
EXP APR 2018

Wa tano:
B13m/D019
E DO 0819

wa sita:
Mfg date Aug 2016
Exp date july 2018
Batch no 0816

Kuna watanzania wenzetu wengi ambao hawawezi kuchanganua huu utitili wa namba, Mpangilio na Lugha inayotumika.

Mamlaka husika liangalieni hili, kwa maana ya kulitafutia ufumbuzi

Naomba kuwasilisha!
 
mada yako ni nzuri kwa tahadhari ya afya zetu. mara nyingi tarehe za kwanza ni za cku ya kutengenezwa bidhaa na hiyo inayofuata ni cku ya kuharibika. ila tambua: EXPIRE DATE maana yake mwisho wa matumizi kwa bidhaa husika na BEST BEFORE DATE maana yake mwisho wa ladha au ubora wa bidhaa husika ila siyo kuharibika kwake.
 
Sawa mkuu!
Kwangu mm siyo tatizo kwa hayo, jamii inayotumia ni pana sana inaweza kujua haya?
Hata mijadala kama hii hawana uwezobwa kushea! Hapo ndo inakuwa shida
 
Kwa kuwa watumiaji wengi wanatumia Kiswahili na pengine hawana uzoefu na vyakula kwenye pakti, basi ingewekwa 'Tumia kabla ya..' au Imetengezwa .., Inaharibika ...
Kwa wasiotumia Kiswahili na nahisi kutokana na asili yao, kwamba wanayajua mambo haya, wataelewa tu kwa kuona tarehe zilizowekwa.
 
Tatizo ni lugha asee, kiswahili hakitumiki kabisa
Nadhani wangeandika mfano hivi:

Itadumu hadi Taerehe 13/07/2018

Kama kuna maelezo mengine yatenganishwe na hiyo sentesi au yawe madogo kuliko
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Kwa kuwa watumiaji wengi wanatumia Kiswahili na pengine hawana uzoefu na vyakula kwenye pakti, basi ingewekwa 'Tumia kabla ya..' au Imetengezwa .., Inaharibika ...
Kwa wasiotumia Kiswahili na nahisi kutokana na asili yao, kwamba wanayajua mambo haya, wataelewa tu kwa kuona tarehe zilizowekwa.
Bidhaa zinapotengenezwa kama ni kwa ajili ya kupeleka nje zinaandikwa kabisa kwamba niza kupeleka nje, shida ipo kwenye hizi bidhaa za ndani.
 
Back
Top Bottom