Mipaka yetu kuvamiwa, vyombo husika viko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mipaka yetu kuvamiwa, vyombo husika viko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by siyabonga, Sep 2, 2012.

 1. s

  siyabonga Senior Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma na kushtushwa na habari ambazo zimeendelea kuripotiwa na gazeti la Nipashe, jana na hata leo { 03/08/ 2012} kuwa maeneo ya mpaka wa Tanzania huko mkoani Kagera yamevamiwa na wahamiaji haramu kutoka Nchi za jirani. Wametulia, hawana wasiwasi, wanafanya mambo yao kama vile wako kwao, na wanatii mamlaka ya Nchi wanazotoka!

  Cha kushangaza, viongozi husika wanakiri udhaifu, wakiwamo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo husika. Kwa nini bado wapo katika nafasi hizo?


  Hii ni hatari, najiuliza kwa nini tunachezewa kiasi hiki? Viongozi hawaoni? Hili kweli ni jambo la kusubiri mpaka Waziri afanye ziara ndio aelezwe? Inakuwaje tunanunuliwa kwa bei rahisi kiasi hiki?

  Napata wasiwasi inawezekana na maeneo mengine ya mipakani nayo yanavamiwa kwa ujinga kama huu na hakuna hatua zinazochuliwa.

  Vita ya kumtoa Nduli Idi Amini ilikuwa ya nini kama hatuwezi kulinda mipaka yetu? Maybe alitumia mkakati mbaya, pengine badala ya kuvamia, angekuja na kitu kidogo akatoa rushwa angemegewa pande kubwa tu la ardhi.

  Kwa nini Waingereza walipigana vita vya Falklands, maelfu ya km kutoka kwao? Kwa nini hawakuwaachia tu Argentina? Kama walipigana kwa eneo dogo la kisiwa,tena liko mbali, na kuna utata wa umiliki, je ukiwasogelea kwao inakuwaje? Kisiwa cha Migingo je? Mbona hao majirani zetu wanaovamia kwetu walitaka kutwangwana? Ni sisi tu ndio hatujui umihimu wa ardhi?

  Viongozi, kaeni chini, chukueni hatua sasa. Mnapuuza viapo vyenu vya kuilinda na kuitetea JMT

  Kama huwezi kuwa na viongozi wanaojali hili, ni bora waondoke mapema. Tusimlaumu Chief Mnagungo wa Msovero, kwa upeo na nyakati za kipindi kile:hakujua analolitenda. Wabaya zaidi ni hawa akina Mangungo wa leo, wanouza Nchi, wakijua wanachofanya, kwa vipande thelathini vya fedha!, Huu ni usaliti, na adhabu yao ni mbaya sana. Sitaki kuingia huko kwenye adhabu za wasaliti, lakini ni mbaya. Yaliyompata Yuda, yatufundishe.
   
 2. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Serikali yetu haiwezi kufanya kazi hiyo kwa sasa,Ila bado inawashughulikia na kuwaua wananchi wake hasa huko nyamongo,Arusha,Morogoro na sasa hivi huko Mfindi wanatarajia kuua watu kwa kutumia kitu kizito kirukacho yaani Flying Object kama walivyosema kwa Marehemu Issa WA Morogoro.
  Askari wetu si kulinda mipaka kama unavyojua.FFU si wa kulinda raia bali kazi kuu waliyokabidhiwa na serikali hii ni KUUA raia kwa visingizio mbali-mbali.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,288
  Likes Received: 19,438
  Trophy Points: 280
  wananjeshi na askari wapo bussy kupigana na chadema
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huko biharamuro, kuna misitu na ardhi nzuri ajabu, unaweza kutembea na gari, kuangalia katikati ya msitu unakuta mtu kafyeka analima na amejenga kibanda chake pale....ni warundu wanalima kama trekta...warundu huku kagera ni kitu cha kawaida, kuna wengine hata kiswahili hawajui kabisaa.wana ming'ombe yao ile ya ankole matajiri na wanawanyanyasa sana watz wakiwaita masikini kwasababu hawana utajiri wang'ombe....wengi wao walipigana vita, hivyo wanajua vizuri kutumia bunduki, wanatumia ujuzi huo kufanya ujambazi wapendavyo...selikali ipo kimya tu.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Wako bize kupora simu za waandamanaji
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Mnadhimu wa jeshi hutoa matamko ya kisiasa, huwa yuko tayari kuwashughulikia chadema nyakati za uchaguzi!! Unapofika wakati wa kuonysha ya kitaaluma kaufyata.
  Tusubiri wakimaliza siasa labda watakumbuka kuulizia, sio kulinda hiyo mipaka sijui manyau.
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  HADI WANYAMA WAMEIKIMBIA RWANDA; JUZI JUZI KWENYE MBUGA PEKEE YA WANYAMA RWANDA... NAONA HII NI FAIDA tutapata WATALII waliokuwa

  Wanakwenda RWANDA...

  NEWS

  Wild animals flee Akagera into Tanzania

  By KABONA ESIARA Rwanda Today

  Posted Saturday, September 1 2012 at 16:57

  IN SUMMARY

  • The Rwanda Development Board said at least 20 per cent of the park was destroyed by the fire, suspected to have been started by poachers 30 days ago.
  • The park is located in eastern Rwanda bordering Tanzania.
  • The fire that started in Nyamatete north of the park four weeks ago was contained last week following a joint effort by police, defence forces and the local community.


  The fierce fire that razed a section of Akagera National Park has forced wild animals to flee to Tanzania.  The Rwanda Development Board said at least 20 per cent of the park was destroyed by the fire, suspected to have been started by poachers 30 days ago.

  The park is located in eastern Rwanda bordering Tanzania.

  A source at the park told Rwanda Today that large part of the park has been destroyed, leaving wild animals with nothing to feed on.

  However, a statement issued by RDB quoting Akagera Management Company said only 20 per cent of the park was burnt.

  “The park management is hiding something. About 80 per cent of the park vegetation was burnt. The areas that was not affected are those surrounding the six lakes and the swamps,” said a source who asked not to be named for fear of victimisation.


  The fire that started in Nyamatete north of the park four weeks ago was contained last week following a joint effort by police, defence forces and the local community.

  To prevent such disasters in future, RDB’s head of tourism and conservation Rica Rwigamba said monitoring teams have been reinforced and numerous fire breaks will be put in place to avoid fire spreading in case of an outbreak in future.

  Mr Rwigamba further appealed to the community near the park to avoid all activities that may ignite any fire, considering that savannah parks are prone to fire outbreaks.

   
Loading...