Hebu tusiwajadili kwanza watafuta kuni
Wawasha moto
Wachochea moto/ wakolezaji
Moto una sehemu tatu pale unapowashwa ama kuwaka
Angalia nyika, pori ama msitu unaoungua..
Kuna moto wa awali.. Huu huwa mwepesi ukipita juu juu na kwa haraka sana.... Hauna madhara makubwa kwakuwa huchoma na kuunguza majani, matawi dhaifu na yaliyokauka sana
Unaofuatua ni moto wa pili... Huu unapita ukikausha kila kilicho kibichi.. Una kasi ndogo
Halafu unaofuatia ni moto wa tatu... Huu ndio ule ambao kuuzima kwake ni shughuli pevu.. Kwakuwa unakuwa tayari ulishasafishiwa njia na kutengenezewa mazingira ya kuunguza kila kitu....
Inawezekana kabisa hii formula ya moto imetumika kwenye siasa za chama tawala... Na ikiwa iko hivi basi kuna akili kubwa nyuma yake inafanya kazi next level
View attachment 1159228
Kuna himaya tatu ziliundwa kwenye huu mfumo wa sasa.. Himaya hizi kila moja ilikuwa na jukumu lake na hazijawahi kuingiliana majukumu(lakini huko mbeleni zitafarakana)
Himaya ya kwanza ilikuwa kazi yake ni kudhoofisha upande wa pili kwa kutumia mgongo wa kuunga mkono juhudi... Hapa zilitumika mbinu zote nzuri na mbaya... Himaya hii imemaliza kazi yake vizuri... Hii tunaiita kama moto wa kwanza
Himaya iliyofuatia ni ile ya bash boi... Kazi yake ilikuwa moja tu... Kuwasumbua kuwatisha na kuwakatisha tamaa wote wenye nguvu kifedha na ushawishi, wafanya biashara na hata wasanii pia.. Huu ulikuwa ni mpango kabambe kuwataka wakae kimya hapo mbeleni... Himaya hii tuliona jinsi wafanya biashara walivyopitia kipindi kigumu... Bila kuwasahua baadhi ya wasanii na watu wenye ushawishi katika jamii... Huu ni ule moto wa pili
Himaya ya tatu ikaundwa... Hii kazi yake ni moja tu... Kuwaandama kwa kila hali wanasiasa walio nje ya mfumo lakini wenye nguvu ushawishi na mvuto... Kuwaandama kwa vitisho, matusi, kejeli na tuhuma mbalimbali... Huu ni moto wa tatu unaounguza vizuri kwakuwa tayari ulishasafishiwa njia.....
Ninini kifuatacho?
Moto wa tatu ndio huwachomoa wale wadudu na wanyama waliojifukia ardhini... Moto huu joto lake ni kubwa.. Hivyo wakijitokeza tu wakimbie fukuto wanakutana na marungu ya clips..... Hivyo ndani hakurudiki
Tunaanza wiki muhimu kwa siasa za Tanzania... Wale wote walio nje ya mfumo na ambao ni tishio tayari faili zao za kila aina ya kashfa zimekamilika... Lakini ilihitaji kuwachokonoa ili sababu ipatikane... Hili limefanikiwa mno... Sasa ni suala la muda tuu...
Mtego uko hapa....
Kila upande kwa sasa una watu unaowaunga mkono kuanzia idara nyeti, vyombo vya ulinzi na usalama mpaka chini kabisa... Ni vita inayohitaji akili kubwa, werevu na utashi wa hali ya juu
Kuna zile himaya tatu zina watu wake pia ambao baadhi wanaweza kugeukana mbele ya safari ama baada ya hapo zikaanza kutunishiana misuli zenyewe kwa zenyewe... Hilo sio la sasa....
Tunaianza wiki muhimu sana tutaona nani ataanza kupiga yowe.... Achana na zile clips hazina uzito wowote lakini zimeshafikisha ujumbe muhimu pande zote... Clips zilikuwa ni kibiritii tuu