Mioto ya aina tatu...

Mioto ya aina tatu...

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,446
Reaction score
829,806
Hebu tusiwajadili kwanza watafuta kuni
Wawasha moto
Wachochea moto/ wakolezaji

Moto una sehemu tatu pale unapowashwa ama kuwaka
Angalia nyika, pori ama msitu unaoungua..
Kuna moto wa awali.. Huu huwa mwepesi ukipita juu juu na kwa haraka sana.... Hauna madhara makubwa kwakuwa huchoma na kuunguza majani, matawi dhaifu na yaliyokauka sana

Unaofuatua ni moto wa pili... Huu unapita ukikausha kila kilicho kibichi.. Una kasi ndogo
Halafu unaofuatia ni moto wa tatu... Huu ndio ule ambao kuuzima kwake ni shughuli pevu.. Kwakuwa unakuwa tayari ulishasafishiwa njia na kutengenezewa mazingira ya kuunguza kila kitu....

Inawezekana kabisa hii formula ya moto imetumika kwenye siasa za chama tawala... Na ikiwa iko hivi basi kuna akili kubwa nyuma yake inafanya kazi next level

IMG-20190721-WA0062.jpeg

Kuna himaya tatu ziliundwa kwenye huu mfumo wa sasa.. Himaya hizi kila moja ilikuwa na jukumu lake na hazijawahi kuingiliana majukumu(lakini huko mbeleni zitafarakana)

Himaya ya kwanza ilikuwa kazi yake ni kudhoofisha upande wa pili kwa kutumia mgongo wa kuunga mkono juhudi... Hapa zilitumika mbinu zote nzuri na mbaya... Himaya hii imemaliza kazi yake vizuri... Hii tunaiita kama moto wa kwanza

Himaya iliyofuatia ni ile ya bash boi... Kazi yake ilikuwa moja tu... Kuwasumbua kuwatisha na kuwakatisha tamaa wote wenye nguvu kifedha na ushawishi, wafanya biashara na hata wasanii pia.. Huu ulikuwa ni mpango kabambe kuwataka wakae kimya hapo mbeleni... Himaya hii tuliona jinsi wafanya biashara walivyopitia kipindi kigumu... Bila kuwasahua baadhi ya wasanii na watu wenye ushawishi katika jamii... Huu ni ule moto wa pili

Himaya ya tatu ikaundwa... Hii kazi yake ni moja tu... Kuwaandama kwa kila hali wanasiasa walio nje ya mfumo lakini wenye nguvu ushawishi na mvuto... Kuwaandama kwa vitisho, matusi, kejeli na tuhuma mbalimbali... Huu ni moto wa tatu unaounguza vizuri kwakuwa tayari ulishasafishiwa njia.....

Ninini kifuatacho?
Moto wa tatu ndio huwachomoa wale wadudu na wanyama waliojifukia ardhini... Moto huu joto lake ni kubwa.. Hivyo wakijitokeza tu wakimbie fukuto wanakutana na marungu ya clips..... Hivyo ndani hakurudiki

Tunaanza wiki muhimu kwa siasa za Tanzania... Wale wote walio nje ya mfumo na ambao ni tishio tayari faili zao za kila aina ya kashfa zimekamilika... Lakini ilihitaji kuwachokonoa ili sababu ipatikane... Hili limefanikiwa mno... Sasa ni suala la muda tuu...

Mtego uko hapa....
Kila upande kwa sasa una watu unaowaunga mkono kuanzia idara nyeti, vyombo vya ulinzi na usalama mpaka chini kabisa... Ni vita inayohitaji akili kubwa, werevu na utashi wa hali ya juu

Kuna zile himaya tatu zina watu wake pia ambao baadhi wanaweza kugeukana mbele ya safari ama baada ya hapo zikaanza kutunishiana misuli zenyewe kwa zenyewe... Hilo sio la sasa....

Tunaianza wiki muhimu sana tutaona nani ataanza kupiga yowe.... Achana na zile clips hazina uzito wowote lakini zimeshafikisha ujumbe muhimu pande zote... Clips zilikuwa ni kibiritii tuu
 
Walijitahidi kuziba watu midomo kwa viroba na risasi lakini wakati unakuja hata mawe yataongea!
 
Huo moto wa tatu unaonekana ni mkali sana, ngoja nipunguze kazi ili saa nne nimsikilize musiba
 
Moto wa tatu unachanganya walokuwamo na wasiokuwamooo...unateketezaaa...hauzimiki hadi mvua ya masika inyesheee.
 
Moto wa tatu unachanganya walokuwamo na wasiokuwamooo...unateketezaaa...hauzimiki hadi mvua ya masika inyesheee.
*MPASUKO WA CCM UMEKARIBIA POINT OF NO RETURN, NI AMA CCM IFE AU MAGUFULI ACHUKUE NAFASI YA CCM (MAREHEMU). CCM ikisha pasuka pande mbili (Makada wote wakubwa waandamizi (ccm asilia) wakishondolewa ndani ya ccm na kwenye serikali) Usalama wa Taifa ndio utakao fuata kupasuka na wa mwisho ni Jeshi la Nchi, na katika mazingira haya, Magufuli hatakuwa kwenye mazingira ya kuweza kuvuka salama na pengine naweza kusema havuki 2020, nachelea kusema Yaliotokea Zimbabwe yanaweza kujitokeza Tanzania; Mark my words.*

*Baada ya kuisikiliza Audio iliyopewa sehemu ya 5 ambayo imehusisha sauti ya Kachero Benard Membe na mwingine atajwae kama mwenyekiti wa kitongoji, ndipo nilipogundua kwamba, kuna kuni mpya zimeingizwa kwenye moto ambao ulikuwa unawaka kwa kusuasua. Maneno yaliotamkwa kwenye sauti ya Membe ni ishara ya vita kamili kuchukua mkondo wake muda si mrefu (No compromising). Tunachokishuhudia sasa hivi ni hatau ya mwanzo wa mwisho wa ccm na kipekee sana Maguguli na wafuasi wake kindakindaki. Hatua ya mgawanyiko wa makada na wananchama waandamizi ndani ya ccm ambapo vita yake bado haijahusisha moja kwa moja nguvu kubwa nyuma yao. Kwa sasa ni Magufuli na vijana wake wakijaribu kutingisha kiberiti ambacho ni (makada asilia wa ccm) tena wao hawatumii jeuti iliyo nyuma yao. Na katika hili ninawashauri sana wale vijana na makada wa ccm ambao hupenda sana kutafuta sifa kwa kuyabeba haya na kujifanya wanajitoa mhanga kumpigania magufuli, wawe makini sana na haswa wale wa upande wa Magufuli, kwasababu hii vita imefikia kuingia Mstari mwekundu.*

*Pamoja kwamba, Magufuli amenza kutumia baadhi ya taasisi za serikali, kujaribu kupambana na ndugu zake ambao ndio waliomweka madarakani bila weledi wa kutosha wa jambo analojaribu kulifanya. Wanaomsaidia magufuli kwenye matumizi haya ya taasisi za umma dhidi ya waandamizi wengine ndani ya ccm, wanamtengenezea angamizo kubwa sana na angamizo hilo linaweza kuleta mushkeri kwa Taifa zima.*

*Taswira ya nje ya vita hii ni kama chama kizima kimeshapasuka, hapana bado, na itakapofikia hapo, basi watu kama magufuli hawawezi kuendelea kuwepo hapo walipo, nasikitika sana kwamba, Magufuli amekosea kuanzisha vita hii mapema sana*

C&P
 
chochea kuni kwa bidii, ngoma ishakubali hii......hadi kieleweke

1563779856598.png
 
Back
Top Bottom