Minziro awakaanga wachezaji JKT

Minziro awakaanga wachezaji JKT

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
257
minziro.jpg


​
KOCHA wa JKT Ruvu, Felix Minziro juzi Jumanne alikaa kikao cha dakika 30 na wachezaji wake baada ya mazoezi yao ya kawaida na kuwataka wachezaji hao waache mzaha na kucheza soka la ushindani litakalojenga heshima ya kikosi hicho.

Minziro alionyesha kukasirishwa na kikosi chake hicho kushindwa kupata ushindi wowote kwenye mechi tatu za kwanza za Ligi Kuu Bara ikiwa imefungwa mechi mbili na kutoka sare moja.

Kocha huyo wa zamani wa Yanga alionekana kuwa mkali kwa wachezaji wake hususan washambuliaji kutokana na kukosa umakini wa umaliziaji kwa nafasi wanazozipata jambo linaloinyima timu hiyo fursa ya ushindi.

"Nataka mcheze mpira, nataka mcheze kwa morali ya juu, kila mchezaji atendee haki majukumu yake, kama ni mshambuliaji uhakikishe unafunga mabao," alizungumza Minziro kwa ukali.

JKT Ruvu itacheza na Prisons Jumapili ya wiki hii jijini Mbeya ikiwa ni mechi yao ya nne ya ligi. Mechi ya mwisho iliyozikutanisha timu hizo, Prison ilishinda mabao 6-1.

MwanaSpoti
 
Huyu sii ndie yule kocha timu yake ikifungwa na yanga anajifanya kukasirika uwanjani kisha akienda chooni anashangilia
 
Back
Top Bottom