Mimi nami nimepita Minako, enzi zile KAMATA inakwenda kule. Nakumbuka sana jinsi KAMATA ilivyokuwa inapata shida ya kupita pale Kinyanyiko! Nakumbuka shida ya Maji.
Namkumbuka Headmaster Mtasigwa, Second master Matu ( na diasater za mkewe alitekuwa mwalimu), na walimu wengine. Namkumbuka Mwalimu Sawaya, ambaye wakati huo walikuwa na TOYOTA STOUT mpya kabisa.
Kiboko zaidi ni yule mmarekani aliyezaa na mke wa mwalimu!
Wakati huo, lami ilikuwa haijafika hata Pugu secondary, yaani magari mengi yalikuwa yanaishia mwisho wa lami!
Hii ilikuwa mwaka 1986-1988!