singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepiga marufuku biashara ya vyakula katika minada yote iliyopo manispaa ya Dodoma.
Amri hiyo ameitoa baada ya kutembelea mnada wa Msalato na kujionea taratibu zilizopo hapo.
Alisema upigaji marufuku wa minada hiyo kunatokana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Pamoja na kutoa amri hiyo baadhi ya wafanyabiashara wamesema watagomea agizo hilo.
Agizo hilo amelitoa jana majira ya saa tisa alasiri katika mnada wa Msalato wakati alipotembelea mnada huo.
Alipowasili hapo alikuta shughuli za uchomaji wa nyama na vinywaji zikiendelea. Alisema staili inayotumika kufanya shughuli katika eneo hilo ni kichocheo kikubwa cha ugonjwa wa kipindupindu .
Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara mnadani hapo wanadai kuwa wanalazimika kuendelea kufanya biashara katika eneo hilo kutokana na ugumu wa maisha licha ya uwepo wa ugonjwa wa kipindupindu.
Wafanyabiashara hao, Sabrina Rajab ,Samson Ibrahim na Ally Mohamed walisema kwamba wanaendesha familia zao kwa kushiriki katika minada hiyo na kitendo cha kuwaambia waache kitawaathiri sana kiuchumi.
Pamoja na wafanyabiashara hao kutoridhishwa na agizo la Waziri Ummy Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Dk Jasmine Tiisekwa alisema anaunga mkono kufungwa kwa mnada huo na kuwaomba wakazi wa Dodoma kutokubali ugonjwa wa kipindupindu kusambaa.
Aidha katika hatua nyingine Waziri Ummy Mwalimu amewataka wananchi kote nchini kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na ugonjwa huo.
Tangu kuingia ugonjwa wa kipindupindu katika manispaa ya Dodoma mpaka hivi sasa watu watano wamefariki kwa ugonjwa huo na wengine 214 walipata ugonjwa na kutibiwa.