Nilikutana na huyu binti mrembo sana mwenye hips la maana mwaka 2006 kipindi hicho tunapambana na tuition k/koo. Kwa bahati nzuri wote tulifanikiwa kufaulu na kuchaguliwa mlimani hapa upendo ulikuwa motomoto kila sehemu tuko nae na ikizingatia tulikuwa na bumu 100%.
Basi tulizunguka sana viwanja na hotel za mjini hadi Africana huko giraffe, jangwani, water world, white sands, escape II, MAHABA beach ununio kote huko. Katika kipindi chote cha masomo mm nilikuwa namsaidia kila kitu kuanzia assignment hadi kupiga kopi madesa kufika mwaka wa pili tukaenda kutambulishana kwetu na kwao pia mambo yalienda vizuri hadi chuo kimeisha, changamoto ikaja kwenye kutafuta ajira na bumu limekata.
Mimi nilibaki kwa kaka yangu sinza kumekucha na binti akasema ngoja akatafute michongo arusha nikamwambia poa. Kasafiri baada ya wiki simu yake haipatikani. Nikapiga simu arusha wakaniambia huyu mtu hajafika kabisa huku tangia amalize chuo. Wakati natafakari cha kufanya siku moja mtu ananipita anaendesha rav4 new model akiwa kafanana na mchumba wangu.
Nikajipa moyo kuwa hawezi kuwa yeye sababu hata kuendesha gari hajui. Mara fb akanitoa urafiki, na whatsup akaniblock, nikajua hapa sasa dalili ya mvua ni mawingu siku nilikutana na roommate wake kwenye harusi flani hivi ukumbi wa ngome ndio akanipa details zote kuwa sasa hivi yuko na motto wa mshua mmoja Oysterbay huko anakula maisha na muda si mrefu atavalishwa pete.
Sikuwahi kunywa pombe maishani mwangu ila siku hiyo harusini nilishangaa tu nimekata castle lite tatu na nkaondoka kabla hata ya chakula ilipita miezi 6, nikapata ujumbe wake ukisema "mambo" nikastuka ila sikujibu kitu baada ya siku 3 dada wa kazi kwa bro ananipigia simu na kuniambia kuwa shemeji amekuja nimemuingiza chumbani kwako. Nikaacha shughuli zangu mjini na kurudi nyumbani ili nimfukuze.
Nimengia room namkuta binti katoa nguo zote yupo kama alivyozaliwa kalala kifudifudi na usingizi umempitinikasema kama ananitega hivi basi hapa amenikosa, nilikaa pembeni kwenye kiti hadi alipoamka sikumgusa hata nywele.
Baada ya kuamka nikamuuliza kulikoni ? Ndio akaanza kuniambia kuwa kakutana na watoto wa mjini, yule jamaa masaki sio kwao aliwekwa tu aangalie nyumba kipindi kaka yake yuko masomoni nje hivyo mwenyewe amerudi na jamaa anaondoka kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine hata yale magari aliyokuwa akipewa demu atembelee jamaa hana hata moja mwisho akaishia kulia. Watoto wa mjini walimuweza ila na mimi sio yule tena.