Mimi si binadamu bali mimi ni mtu tu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,695
149,921
Eti mpaka leo nahitaji mtu apige kampeni kunielimisha kuwa chama fulani hakifai.

Ningekuwa binadamu kweli ningehitaji kampeni kunishawishi kuwa chama fulani hakifai?

Katika hili binadamu wala haitaji kampeni bali wanaohitaji kampeni ni watu.

Na baada ya yote haya,"watu" watajisifu na kushangilia lakini "binadamu" watawahurumia na kuwashangaa.

Binadamu ni wachache lakini watu ndio wengi na hili ndio tatizo.
 
jg.PNG
 
Tuma kwa cdm hii msg haraka ili warudishe mtandaoni ile list of shame ili usihitaji kampeni wala ushawishi.
 
Viongozi wa UKAWA nao ni watu tu na wala sio Binadamu. Hawaoni kuwa kushiriki uchaguzi katika sheria hizi ambapo wasimamizi na waidhinisha matokeo ni wateuliwa wa Mwenyekiti wa CCM ni kupoteza muda tu?? Watu hawa wala hawaoni kuwa nguvu kubwa sasa ingewekezwa kwenye madai ya Katiba mya na wala sio ile pendekezwa kama wanataka mabadiliko?? Watu hawa wana macho wala hawaoni hilo. Wana masikio wala hawasikii hilo. Ni watu kwelikweli!!!
 
Kama ungekuwa karibu ningekuagizia ya baraidi unayoitaka, mkuu ujumbe wako ni muhimu lakini hakuna atakayekuelewa sababu hapa pia Binadamu kama ninyi ni wachache hapa Jamii forums. Miaka ya 90 wakati vyama vingi vinaanzishwa lengo kubwa lilikuwa ni kudai Katiba na ndiyo chanzo cha NCCR, lakini CCM waliwazidi ujanja kina Mapalala na Kasanga Tumbo, wakawapandikiza watu wao kama Mzee Mtei, Mabere Marando. Masumbuko Lamwai na wengine wengi. NCCR ikabaidlishwa kutoka daraja la kuombee ama kudai katiba mpya na kuwa chama cha siasa. Watu kama kina Mapalala na mzee Fundikira walioipigania vyama vingi tangu miaka ya 64 mzee Nyerere alipobadilisha katiba na kuifanya ya chama kimoja na kuwaweka vizuizini kina Mapalala walizidiwa ujanja na ccm kupitia vibara wao ambao mpaka sasa ndiyo viongozi wakuu wa upinzani.

Kama ulikua na umri wa miaka 18 na kuendelea wakati na ulikua unafuatilia siasa za Tanzania utaelewa kwanini baadhi yetu humu ndani tunajua kuwa hakuna upinzani wa kwelio bali tuna waganga njaa na mamluki wa CCM.

NCCR kirefu chake ni The National Convention for Construction and Reform, sasa jiulize kitu gani walicho reform mpaka sasa zaidi ya uyoga wa vyama?
 
Eti mpaka leo nahitaji mtu apige kampeni kunielimisha kuwa chama fulani hakifai.

Ningekuwa binadamu kweli ningehitaji kampeni kunishawishi kuwa chama fulani hakifai?

Katika hili binadamu wala haitaji kampeni bali wanaohitaji kampeni ni watu.

Na baada ya yote haya,"watu" watajisifu na kushangilia lakini "binadamu" watawahurumia na kuwashangaa.

Binadamu ni wachache lakini watu ndio wengi na hili ndio tatizo.
Hahaha........ Idadi ya watu ni kubwa kuliko binadamu?
 
Back
Top Bottom