jukiha
Member
- Jan 9, 2017
- 72
- 27
MIMI RAIS MAGUFULI naleta ombi langu kwako ukiwa kama kiongozi na mfanya maamuzi yote makubwa, Mimi Ni kijana katika taifa lako nimehitim chuo kikuu Ni miaka mitatu sasa imeisha ajira za serkali hamna na kauli yako kuu tujiajiri ,pamoja na kuwa nimesomeshwa na mama yangu mjane kwa kukaanga chapati ambaye hakuwa na msaada kwangu zaidi ya elimu nilijitahidi na kuhitim chuo kikuu mama hakuwa na mtaji wa kunipa nikajiajiri nilitumia jitihada zangu nikapata mtaji nikajiari katika kilimo lakin nilipata hasara kubwa kutokana na solo la zao La nyanya kuwa bovu na faida kidogo niliyopata iliishia kwenye matibabu ya mama baada ya kuanza kuugua cancer ya Shinto ya kizazi na juzi nimemzika baada ya kupoteza Maisha bila kuonja matunda ya mwanae aliyemsomesha kwa kuungua kupika chapati hapa nimebak na wadogo zangu wananitegemea mimi na sijui hata nawasaidiaje mana kilimo mtaji sina tena na kila napotuma maombi yakazi naambiwa walim wapo wa kutosha ,najua tupo yatima wengi kama Mimi na wengine wenye matatizo labda hata zaidi yangu na elimu tunayo naomba mtusaidie kupaza sauti japo serkali itusikie tupate kuajiriwa chaguzi hizi zipungue ili na sisi wanyonge tupate ahueni ,mkinisaidia kusambaza ujumbe huu umfikie raid wetu nitawashukuru sana ASANTENI