MIMI NI MSAKA TONGE

monotheist

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
887
Reaction score
1,596
Habari wakuu, natumaini hamjambo
Nami pia ni mzima wa afya,
Mimi ni kijana wa kiume mhitimu wa
kidato cha sita mwaka 2016 nimeshindwa
kuendelea na elimu ya juu sababu ya
kukosa pesa ya ada na sina uhakika kama
nitaenda chuo maana kila kukicha ni
afazali ya jana kwa kweli maisha ni
magumu mno.
Nina cheti cha hotel natafuta kazi ya hotel
naweza kufanya kazi katika nafasi
zifuatazo
1.hotel receptionist
2.House keeping
3.Porter
4.Launder
Kwa yeyote atakayeguswa tuwasiliane PM
mimi ni mkazi wa Dar es salaam na
nipotayari kufanya kazi mkoa wowote
hapa Tanzania.
Mungu awabaliki mlioacha shughuli zenu
na kuamua kusoma uzi huu.
NATANGULIZA SHUKRANI.
 
Nakushauri fikiria zaidi kujiajiri hata kwa kuuza Karanga za kukaanga,Siku hizi kazi za hoteli zimekuwa changamoto kubwa kupata kutokana na hoteli nyingi kukosa wateja.
Siku hizi utaona hoteli ina wafanyakazi wachache ambao ni multi purpose.
Any way kila la heri!!
 
Write your reply...Ahsante kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
Kama upo kijijini na huwa mnabustani jaribu kilimo cha bustani kama mchicha, nyanya, nyanya chungu, sukuma wiki n.k utapata pesa mkuu. Achana na mambo ya kuajiliwa hasa kwa fani ulizo orodhesha hapo juu. Waweza jaribu na ufugaji pia
 
Ahsante mkuu ila nilishathubutu kufuga kuku chotara nilipata changamoto nyingi sana hatimae nimepoteza hata pesa ya mtaji
 
Ni kweli dereva ndiyo mpishi
 
Mkuu natumia tecno p3 hii simu inamatatizo kama yote yaan natumia kwa ajili ya kupiga, kupokea simu, kutuma sms na kufungua operamini tu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…