Mimi ni CCM damdam lakini nimependa kiitikio cha CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimi ni CCM damdam lakini nimependa kiitikio cha CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eghorohe, May 18, 2012.

 1. Eghorohe

  Eghorohe JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nilipita uwanja mmoja huko mbezi kwa msuguri uwanja ambao Juma Kaseja huwa anafanyia mazoezi binafsi kwani upo karibu na bangaloo lake,timu moja ya watoto ilifunga wenzao wakashangilia sana,mtoto mojawapo wa timu iliyofunga bao akaita kwa sauti CHADEMAAA! wote wakaitikia kwa pamoja KAMATA MWIZI MEN ! nilipo uliza mwizi ni nani? nikaambiwa ni mafisadi + wezi wa kura kwenye uchaguzi! dah kwa kizazi hiki patachimbika hapo siku za usoni!
   
 2. S

  STIDE JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu usishangae!! M4C ipo kazini!! CCM wanakimbia vivuli vyao!!

  Nimeipenda hii pia!!
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Hapa point ni Mapenzi uliyonayo kwa CCM, mtu mzima unasema wewe na kitu fulani ni DAMDAM, watu kama nyie hata tukibadilisha katiba mara mia moja mtaendelea kuwavuta wenzenu mashati kwenye harakati za kutafuta unafuu wa maisha.

  Hao wanaojurikana kwamba wanafaidika na mfumo mbovu wa uongozi kwenye Taifa letu sasa wanaogopa kujitaja kwamba wanaipenda CCM wamebaki kudai wanajivua Gamba, Moja ya msingi wa hoja ya kujivua Gamba ni kutuma meseji kwa watanzania kwamba hata wao wanajua kwamba chama chao kimeoza na kwamba sasa wanachukua hatu za kukisafisha, siku za karibuni zaidi wameanza kusema kwamba Chama hicho kisipobadirika kitapoteza dora, Hawawezi hata kidogo kusema kwamba wao ni nambari one wala nini sijui

  Wewe unaibuka na kusema eti wewe ni CCM DAM DAM.

  Acha Mungu aumbe wazima na vilema aisee
   
 4. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wauza chai JF napo wapo:baby:
   
 5. mashami

  mashami Senior Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  uliyeta huu uzi ushajua maana ya ukombozi nakushauri uende ofisi ya chadema iliyo karibu na wewe uchukue kadi ukiwa na passport 2,karibu kwenye ukombozi wa kifikra na kimaendeleo...peepoz!!
   
Loading...