JJ10
JF-Expert Member
- Jan 13, 2014
- 282
- 133
Habarini wanaMMU!
Ivi ulishawahi kutafakari na kujiuliza ni mfumo gani unaotumia kuendesha maisha yako ndani ya ndoa?
Kama hujui basi huu ni mda mwafaka wakuliangalia hili' huenda ikaboresha maisha yako ya ndoa.
Maisha ndani ya ndoa yana mifumo mitatu. Kama ifuatavyo;
A) Mfumo Dume - mfumo huu ulitumiwa sana enzi za mababu zetu. Yaani baba ndo kichwa cha familia, baba ndo mwamuzi mkuu na ndo msemaji wamwisho wakila jambo linalohusu familia. Kwenye mfumo huu ndoa zilidum sana, maadili yalizingatiwa na kulikuwa na nidhamu ya hali ya juu katika familia hadi jamii kiujumla. Paka hivi sasa mfumo huu inaendeshwa na familia chache sana.
B) Mfumo wa Usawa - huu mfumo umeanza miaka ya hivi karibuni na paka sasa unazidi kushika kasi ya ajabu. Kwenye mfumo huu mwanaume hafanyi jambo bila kumshirikisha mkewe' na mwanamke vivyo hivyo! Hii ni matokeo ya haki sawa inayohubiriwa na mataifa ya magharibi na kupokewa na wanawake wakiafrika bila kuangalia athali za hiyo katika maisha ya baadae. kwenye mfumo huu ndoa zinalegalega sana na nindoa chache zina amani. Ingawa wanawake wanaupenda sana huu mfumo.
C) Mfumo jike - huu mfumo maisha yanaendeshwa na matakwa ya mwanamke ndani ya ndoa! Atakalotaka mwanamke ndilo litakalotekelezwa' baba ni muitikiaji na mtekelezaji wa maamuzi ya mama! Ndoa za namna hii zipo na zinaendelea kuwepo ingawa nivigumu sana kuzitambua kwa nje' paka uingie ndani sana au utokee mtafaruku ndo afunguke.
Vile utakavyoishi na mtu wako toka mkiwa wapenzi au mwanzoni mwa ndoa yenu ndivyo mtakavyoishi maisha yenu yote! Ni vigumu sana kubadilisha mfumo ndani ya ndoa' na ndoa nyingi zinavunjika pale mtu anapotaka kufanya mabadliko ya haraka baada yakugundua kwamba mfumo alioanzisha sio sahihi.
Ushauri; Ukiwa kwenye upenzi, uchumba au ndoa changa DON'T PRETEND' uwe wewe mtu akujue vizuri mapungufu na mazuri yako! Apime na anavofanya maamuzi asije yajutia baadae. Ukipretend alafu baadae unaanza kuonyesha tabia zako halisi kama surprise lazima ndoa iyumbe kama si kuvunjika kabisa. Hii itawafaa na kuwasaidia wenye mahusiano yenye tija na wenye malengo yakuishi maisha yafuraha ndani ya ndoa zao.
Umechagua mfumo upi kwenye ndoa yako?
Wewe ambaye bado ungependa kutumia mfumo upi?
Karibuni kwa mchango, kukosoa, au lolote lile unalojiskia kulisema.