Mimi Mwalimu wa Elimu ya Awali (ECE) natafuta nafasi ya kufanya kazi ya kujiolea kwa miezi 6

Kigorohe

Senior Member
May 21, 2019
160
253
Habari,

Kama mada ilivyotajwa hapo juu, mimi ni mtaalamu wa elimu ya awali ambaye bado nipo masomoni nikisoma Bachelor Degree. Nimeona ni vizuri kabla sijamaliza kusoma nitafute shule ili niwe nafundisha kutafuta uzoefu.

Kwa yeyote ambaye anahitaji au anajua shule yenye uhitaji wa mwalimu wa elimu ya awali kwa mkoa wa Arusha naomba tuwasiliane PM.Mimi nipo Arusha kimasomo napenda kujitolea kabla sijamaliza chuo.

NB: Pia naweza kufundisha course zinazotolewa College zinahusiana na Elimu ya Awali.

Karibuni sana
 
Maliza kwanza, watu wa BED ECE wako wengi sana mitaani, nafasi yako itakuwepo kwa wakati huo, acha kwa wale waliobahatika kupata sehemu za kujishikiza waendelee.
 
Maliza kwanza,watu wa BED ECE wako wengi sana mitaani,nafasi yako itakuwepo kwa wakati huo,acha kwa wale waliobahatika kupata sehemu za kujishikiza waendelee.
Kwahiyo hali ni mbaya mpaka kwa hiyo program mkuu?
 
Tanzania Rural Empowrnment Organization-TAREO, Nia asasi isyo kuwa ya kiserikali yenye makao yakee makuu Moshi,Kilimanjaro.
Asasi hii inafanya kazi na jami hususani za vijijini.
Tunapenda kutangaza nafasi ya kujitolea kufanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ,sita au mwaka mmoja (3-12 ) katika vituo vyetu visuatavyo.
1. SHULEYA AWALI NA KITUO CHA VIJANA MAJENGO,MOSHI (Hii bi shule inayo fundisha watotot wadogo wa kati ya miaka 2-6
Tunahitaji waalimu wa kujitole.
2. MAJENGO VOCATIONAL TRAINING CENTRE, Ni kituo cha mafunzo ya ufundi stadi ,kilimo na ujasiriamali.
KINATOA MAFUNZO KWA AKINA MAMA,VIH=JANA NA JAMII ZA KATA ZA kahe.
3. MOSHI INSTITUTE OF TECHNOLOGY-MIT,CHO CHA UFUNDI STADI NA TECHNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILINO,Kipo moshi mjini.
4.HIMO ICT CENTRE;
Hiki ni kutuo cha mafunzo ya TEHAMA ,huduma za internet na stationary, kulicho HIMO-MOSHI
KWA YEYOTE ATAKAYE PENDA WASILIANE NASI AU ATUME BARUA NA CV ZAKE KWA EMIAL...info@tareo-tz,org au simu no.
o717157659/0754469894.
Kwa wanaohitaji watume CV zao kwa email:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…