Mimi mjazito napata maumivu kwenye makalio

miss chuga

JF-Expert Member
Dec 25, 2019
303
651
Habari za muda huu poleni na majukumu,

Mimi ni mjamzito miezi 3 napata maumivu kwenye makalio yanashuka Hadi kwenye muunganiko wa makalio na mapaja kwa nyuma yani ni kama maumivu yanatokea kwenye misuli iliyopo ndani ya makalio nashindwa Hadi kutembea vizuri, Leo nimeenda hospital doctor kaniambia nipime uti nimepima Sina ameishia tu kuniambia nifanye mazoezi.

Naomba mnisaidie kwa anayefahamu shida itakuwa nini au kwa ambaye alishapata hii changamoto na Mungu awabariki.
 
Hiyo inaweza kuwa sciatica japo mimba bado ni ndogo, ni hali ya kawaida inawapata baadhi ya wajawazito.Hivyo unaweza fanya massaging ya mara kwa mara, epuka kusimama muda mrefu.

Pia hakikisha unapata choo laini ipasanvyo kwa kula mlo kamili Kwani mjamzito pia unaweza usipate choo kama kawaida yako kutokana na physiological changes.

Unaweza hisi maumivu au wakati mwingine kama shoti ya umeme.

Maumivu yakiwa makali sana unaweza ukahitaji dawa za kutuliza, hivyo utapaswa kuwasiliana na daktari ili uweze kupata dawa sahihi ambazo hazitamdhuru mtoto.
 
Habari za muda huu poleni na majukumu, Mimi ni mjamzito miezi 3 napata maumivu kwenye makalio yanashuka Hadi kwenye muunganiko wa makalio na mapaja kwa nyuma yani ni kama maumivu yanatokea kwenye misuli iliyopo ndani ya makalio nashindwa Hadi kutembea vizuri, Leo nimeenda hospital doctor kaniambia nipime uti nimepima Sina ameishia tu kuniambia nifanye mazoezi. Naomba mnisaidie kwa anayefahamu shida itakuwa nini au kwa ambaye alishapata hii changamoto na Mungu awabariki.
Kamuone Physiotherapist
 
Hongera na pole
ukisikia Uchungu wa mwana aujuae mzazi basi huo usemi ndio unaanzia hapo kwenye hayo maumivu
Asikwambie mtu mtoto raha lkn pia anauma

Sasa ushakuwa mwayego unaenda kuwa Mwanamke kamili
VUMILIA dada
Asante ngoja tu nivumilie hamna namna
 
Back
Top Bottom