Maumivu niliyonayo najuta kuingia kwenye mapenzi, nifanye nini?

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,955
6,885
Ukirejea katika Uzi huu > Nahisi mke wangu anani-cheat, nifanye nini kumkamata?

Ambao ni Uzi nilieleza jinsi mke wangu alipoanza kunicheat, Leo ni week ya 4 Sasa, Nimekuja na Muendelezo wa yaliyojiri baada ya Shauri nyingi zilizotoka kwenu wadau, Ushauri niliofanyia kazi ilikuwa wa Ugumu wangu ambae alinishauri nitenge muda wa kukaa na yule mwanamke then nimuulize kama ana malengo gani na Mimi na je, anaweza kuachana na huyo jamaa anaetaka kuanzana nae au lah?, Majibu yake yalionesha kukiri na kuahidi kuachana na jamaa yule Tena akilia sana, Jambo ambalo lilifanya nirudishe moyo wangu nyuma na kumsamehe huku nikizingatia jinsi tulivyotoka mbali pia, Nilimsamehe na Onyo Kali sana kuwa akirudia basi tutaachana.

Baada ya week moja nilimuuliza "Vp yule jamaa umefanikiwa kumkwepa au bado anakusumbua?" Hapo tushaanza kusahau kisa chote Tena nikiamini kuwa hawana mawasiliano Tena, Mwanamke yule alinijibu "Sijui" Aisee jibu lake liliniumiza na kunifanya nirudi kwenye wasiwasi Tena "Hujui??" "Ndio sijui, kwani we unahisije" Dah! kauli Ile ilinipa hasira nikajikuta nimechukua cm yake kuangalia je bado wanawasiliana?

Kurupushani ilianza kwani hakutaka niguse Simu yake ndipo nilitumia mabavu kwa kumpiga kibao Kisha nikaingia kwenye Call log na kukuta ni kweli kuwa bado wanawasiliana Tena wanaongea dk 10-15 japo namba haikuwa kaisave ila namba ya jamaa niliikariri Kutoka siku ya Kwanza Dah Jambo lile lilinipa hasira Hadi nikapasua Simu ya mke wangu, Kisha nikamgeukia kumuuliza kwanini ananifanyia vile, Yeye alijitetea kuwa jamaa ndie anaempigia, "Lakini kwani hukumuambia umeolewa???" "Hata kama ni boss wako je dk 10-15 mnaongea Nini Tena ubaya tarehe inaonesha hata Jana jumapili ni siku ya kazi lakini mmeongea zaidi ya dk 10 je, unaniona Mimi mtoto???"

DAH! Akili yangu ikaanza kunilaumu kwanini sikufuata Ushauri wa kuachana nae Ila Mwanamke yule alinituliza kwa kuniambia jamaa hua anaempigia kwa kuwa bado ana namba yake ila kwa kuwa nimeshapasua Simu yake na laini nimevunja basi atasajili nyingine na kununua Simu nyingine alafu nitathibitisha Hilo kwa kuwa Sasa jamaa hatokuwa na namba yake mpya, basi nilikubali kumsamehe Tena.

Baada ya siku tatu mwanamke akanunua Simu nyingine na kusajili namba mpya, ila Cha kushangaza alinunua smartphone yake, line mpya ambayo hata namba sikuijua Kisha akaweka patten kwenye lock screen,

Duh! nikaanza kuwa na wasiwasi Tena, kweli mtu anaetafuta uaminifu kwa mtu aliemkosea kiasi kile kwanini anafanya hivi mbona mwanzo tuliwekana wazi Kila kitu, Nilipomuuliza alikuwa Mkali " Bwana nishabadili namba mpya Hana namba yangu Wala Sina yake Kila mtu kwa Sasa abaki na password za simu yake tuaminiane hivyohivyo tusichunguzane" Basi maneno Yale yalizidi kunipa wasiwasi sana kutaka kujua ni kwanini amefanya vile? Je kweli ameachana na yule jamaa?

Akili iliyonijia nilipamua kwanza kuchukua namba yake mpya aliyosajili bila yeye kujua, Kisha siku iliyofuata nilienda kusajili namba mpya Kisha niliinganisha WhatsApp Kisha nikaisave namba yake mpya kucheki WhatsApp nikaona nikaanza kumchatisha kama vile ni yule jamaa na majibu yalikuwa hivi

Mwanamke alionesha kumlalamikia jamaa kuwa anataka kuishi mbali na mimi kwani nimegundua Kila kitu hivyo namnyima amani.

itaendelea.....

Ngoja nilie kwanza maana maumivu niliyopo nayo Aisee najuata kuingia mzima
 
Ushauri wangu kwako
Achana nae
Narudia tena
Achana nae
Achana nae
Na kwa wengine
Ukigundua mke/mpenzi wako ana mahusiano au kuelekea kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine
Achana nae
Hiyo ya kusema atajirekebisha unajidanganya.
Ushauri Achana Nae usije tafuta murder case
 
Ungeficha namba ya simu hiyo iliyotokea katika convo na DP ya Marriana.

Humu pia sio sehemu salama na inaweza kukuletea matatizo mengine.
 
Aiseeh pole Sana Kuna Uzi wangu humu embu jalibu kuupitia naamini utakufunza kitu.hiyo Ali niliipitia maumivu yako nayatambua,Jambo muhimu ni kuamini ajakupenda wewe piga moyo konde maisha hayatupi tunachokitaka Ila tunachokistaili.
 
Kama wewe ni mr huruma basi endelea kuishi nae, ila tambua iko siku ya siku itakuwa aidha wewe au yeye au wote kwa pamoja tutajasikia tukiwa hai kuwa "TUKIO LIMESABABISHWA NA WIVU WA KIMAPENZI", jihadhari bro, jiulize kwa nini yakufike hayo na kwa nini yawe na uwazi wa kiasi hicho!, ni dhahiri muumba anakuonyesha mlango ulio uingia si wako tumia muda huu kutafuta wako kwa amani.
Usilazimishe ng'ombe kunywa maji atakupiga teke au pembe ukae ukiugulia wakati yeye anakula majani na kunywa maji yake raha mustarehe
 
Wewe ni wa dar bila shaka.
Kaka usimuone mjinga, mambo haya hayana fundi! iko siku utakuja kumuelewa ninavyo amini mimi jamaa yuko katika process ya kumuacha huyo mwanamke bila yeye kujuwa sababu sasa hv anachofanya ni kujaribu kufikiri kuwa atambadilisha lakini anajidanganya hatofanikiwa hivyo kitendo cha kudanganywa danganywa mara kwa mara moyo wake utapata sugu na mwisho atafikia maamuzi yasiyo na maumivu kwake kuwa sasa IMETOSHA na hapo atakuwa salama! kwa sasa hvi hana ubavu wa kumuacha huyo dada au mke wazeee!!!!
 
Back
Top Bottom