Mimi mjamzito napata maumivu wakati wa tendo la ndoa

miss chuga

JF-Expert Member
Dec 25, 2019
303
651
Habari zenu?

Naombeni msaada wa dawa au ushauri kwa anayefahamu chanzo Cha tatizo langu, Mimi ni mjamzito wa miezi 2 Ila tatizo langu kila nikikutana na mme wangu napata maumivu makali yani nakuwa Kama vile na vidonda pia baada ya tendo huku chini kunakuwa kunawaka Moto inabidi nijimwagie maji ya Moto ili kupoe wakati mwingine pia napata muwasho.

Nilienda kwa doctor nikapewa dawa ya kuingiza huku chini kwa siku 6 inaitwa cloritimazole nimemaliza kutumia lakini shida iko pale pale. Naombeni mnisaidie tatizo linaweza kuwa ni nini pia ni dawa gani nitumie ambayo haina madhara kwa mjamzito.
 
Kitaalamu linaitwa dyspareumia au post coitus!! Ni tukio ambalo linaweza kusababishwa na wadudu mbali mbali like neisseria gonnoccoci au chlamydia trachomatis and other anaerobs bacteria!

Inaeza ikawa ni PID complications na inatakiwa uende hospitali ili ukapimwe vyema complications (sterility, menstrual irregularities, ectopic pregnancies au tubo ovarian abscesses) inaeza ikawa pia bacterial vaginosis yeast infections au vaginitis)) jitahidi usipate severe complications ikakuletea karaha
Ngoja waje wanaojua
 
Habari zenu? Naombeni msaada wa dawa au ushauri kwa anayefahamu chanzo Cha tatizo langu, Mimi ni mjamzito wa miezi 2 Ila tatizo langu kila nikikutana na mme wangu napata maumivu makali yani nakuw a Kama vile na vidonda pia baada ya tendo huku chini kunakuwa kunawaka Moto inabidi nijimwagie maji ya Moto ili kupoe wakati mwingine pia napata muwasho. Nilienda kwa doctor nikapewa dawa ya kuingiza huku chini kwa siku 6 inaitwa cloritimazole nimemaliza kutumia lakini shida iko pale pale. Naombeni mnisaidie tatizo linaweza kuwa ni nini pia ni dawa gani nitumie ambayo haina madhara kwa mjamzito
Kwahiyo umeshindwa kuvumilia mpk ujifungue...
 
Ila kama tukio hilo halipo wakati huna ujauzito pia nenda clinic ukapime STIS usije mpata mtoto asie na nywele!! Go with ur partner if linajirudia kila ujauzito go consult ur gynaecologist
Kabla ya ujauzito halikuwepo pia kliniki naskia sijui natakiwa nianze na miezi mitatu, hivi siku ya kwanza kuanza kliniki si ndiyo napimwa kila kitu na baba mtoto au inakuwaje?
 
Mimi kuvumilia naweza tatizo nahofia mme Wangu ataishije bila kupewa chakula chake nisije nikamfanya akaanza kutamani vya nje nilaletewa magonjwa
Kibinadamu tuu kumnyima mwezi wako tendo la ndoa haliingii akilini. Pia kuna faida zake pia kitaalam halafu kama hujiskii kulifanya unamwambia kimahaba na atatulia ila sio kila wakati!! Tendo la ndoa linaruhusiwa kabisa wakati wote wa ujauzito wako ali mradi unajiskia kulifanya!! (Natural oxytocin) from men's sperm also refreshing loving and enjoying others says it makes the vaginal oppening goes smoother on delivery!!
 
Kabla ya ujauzito halikuwepo pia kliniki naskia sijui natakiwa nianze na miezi mitatu, hivi siku ya kwanza kuanza kliniki si ndiyo napimwa kila kitu na baba mtoto au inakuwaje?
Unapojigundua ni mjamzito haraka fika kituo cha afya tunatangaziwa redioni kila siku.
 
Back
Top Bottom