Da! Wanawake jamani akili nyingine zitawaletea matatizo
"Eti nilikuwa natania"
Kuna vichwa havitaniwi mambo yaliyo siriasi,tafuteni aina ya utani maana akili ya mwanadamu hubadilika dakika hadi dakika.
Kwa akupendae kwa dhati kauli yoyote ina maana.Nimewahi kushudia rafiki yangu alipigiwa simu na mchumba wake akimwambia anamkaribisha kwenye harusi yake angeolewa karibuni.Rafiki yangu akamuuliza maswali mawili matatu,akampigia simu na rafiki wa mchumba wake (kumbe walikuwa wote) nae akasema ni kweli ataolewa.
Rafiki yangu alichofanya alimtakia kheri,akakata simu akabadili namba,akajuta na kwa hasira akaoa msichana mwingine.
Miezi miwili baadae yule mchumba wake kafanya safari ya ghafla,kakuta jamaa ana mke,alipoulizwa kuhusu ndoa yake akasema"ETI NILIKUWA NAKUTANIA"Ikala kwake
Utani uwe na mipaka
Ushauri:
Mvutie subira Kaka,,bado anahakikisha upendo wako!!