Mimba mashuleni - kilimanjaro

davimsu

Member
Mar 28, 2019
13
4
Hai,Wanafunzi wa tatu wa shule ya Sekondari Sawe Kijiji cha Sawe Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wamesimamishwa shule baada ya kubainika kuwa wajawazito

Mwenyekiti wa Kijiji cha hicho Emanuel Mushi akizungumza na waandishi wa habari alisema watoto hao wameshapewa barua za kusimamishwa masomo

Hawa wanafunzi waliomepewa ujauzito mwaka huu wa 2019,ni wa kidato cha nne mmoja na mwingine kidato cha pili kidato cha tatu hawa waliowapa ujauzito huo wamekimbia baada ya kupata taarifa kuwa wanatafutwa

Mushi,alisema mmoja ya waliokimbia ni msaidizi wa mwalimu mkuu wa shule hiyo(Solomoni Sirikwa) ambeye pia inadaiwa kumpa mimba mwanafunzi mmoja wa shule hiyo nae alikimbia baada ya tukio hilo

Aidha alisema katika shule hiyo mwaka jana hakukuwa na mwanafunzi aliyepata ujauzito ila mwaka juzi 2017 kulikuwa na wanafunzi watatu waliopata ujauzito

Tulikuwa na kikao juzi na wazazi kila mzazi tulikubaliana akiona dereva bodaboda amesimama na mwanafunzi amripoti katika ofisi ya kijiji ili waweze kuchukuliwa hatua kwa sababu ni waharibifu sana kila mzazi amsimamie mtoto wake vizuri na kuwepo ushirikiana wa wazazi na walimu

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Secilia Kullaya, alikiri kuwepo kwa wanafunzi hao waliopata ujauzito

Wakati huo mwanafunz wa darasa la saba(12) shule ya msingi chekereni Kijiji cha Chekimaji Kata ya masama Rundugai amepata ujauzito kwa mujibu wa mwenyekkiti wa kijiji hicho Selemani Juma

Mwenyekiti huyo anadai kupata taarifu kutoka kwa waandishi wa habari kuwa katika shule ya msingi Chekereni kuna mwanafunzi wa darasa la saba amepata ujauzito ndiyo akapata jukumu na kumuuliza mwalimu mkuu wa shule hiyo amapa alikiri kuwepo kwa wanafunzi huyo

Hizi taarifa sikuwa nazo wala ofisini kwangu baada ya kupata taarifa kutoka kwa waandishi wa habari ndiyo nikapata jukumu la kumuuliza mwalimu mkuu wa shule hiyo na kukubali kweli kuna mwanafunzi huyo



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana. Mh rais alishasema hasomeshi wajawazito. Tuunge mkono rais wetu kwa vitendo
 
Hapa ukiwa na mtoto wako wa kike halafu ndio ameshavunja ungo lazima uwe na mahasira tu kila wakati...
 
Back
Top Bottom