Mimba inataka iwe chuma ulete

choupa moting

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
1,508
2,554
Wakuu habarini za mchana,

Kuna mdada nilidate nae few months ago lakini kutokana na baadhi ya mambo kutokwenda sambamba mimi nikaomba tuachane.

Sasa baada ya muda kidogo ananiambia ana ujauzito wangu nikambishia akaenda kupima na majibu yakaja kwenye tarehe zile zile ambazo ndio ilikua mwisho wa mimi kukutana nae kimwili lakini cha ajabu ikawa huyu binti anapata zile siku zake kitu ambacho kikanishangaza ni mimba gani hii?

Ikabidi nimpeleke sehemu kwa mtaalamu wangu tufanye utra sound. Tukafanikiwa kufanya hilo na vipimo vikaonesha kweli mimba ipo lakini iko nje ya kizazi ambapo daktari akapendekeza kwa usalama wa mama mimba ile inatakiwa itolewe na gharama yake ni laki moja na nusu (150000).

Tukapanga kwenda kuiondoa baada ya siku tatu ambapo mambo yangu ndio yangekua mazuri kipesa daktari akasema poa haina shida after three days you just come. Wakati ikiwa ni siku ya pili tu yule dada alizidiwa usiku akiwa kwa dada yake maeneo ya katikati ya jiji na kulazmika kuwahishwa hospitali faster maana tumbo lilikua likimkata vibaya ila sio hospitali ile ya mwanzo niliyompeleka mimi.

Nilipigiwa simu majira ya saa 2 usiku na dada yake nikaambiwa mwenzio yuko hospitali yupo hoi basi nikajiandaa zangu nikafika hospitali kumjulia hali. Nikamuona daktari akaniambia nimpe laki amalize mchezo usiku ule. Yaani mpaka saa tisa usiku niko pale mpaka zoezi linamalizika.

Hatima ya tukamaliza na daktari akanihakikishia mwanamke yuko salama. Basi nikawapeleka kwao nami nikaenda zangu kwangu.

Asubuhi kama kawaida nikamjulia hali na kumtumia pesa za kuimarisha afya, nimefanya hvyo mpaka aliporudi kwenye afya yake ya kawaida.

Sasa kinachonishangaza ni kwamba kila siku ananipigia anataka hela tuu kitu ambacho naona km ananifanyia fix wakat ameshapona. Ukimtumia sasa hivi labda elfu 15 jion anapiga tena anataka hela. Nikimwambia sina ananiambia kumbuka mimi ni mgonjwa wako. Halafu ujinga mwingine anaoufanya nikimpigia mimi simu anakata mpaka apige yeye yaani anajifanya yuko busy. Dah imekua tabu tena.

What should i do nipeni mawazo jamani. Ananivuruga huyu.
 
Acha ujinga ww kama umeshamaliza tatizo hela unamtumia ya nn tena mkaushie tu
 
Kwani si mlishamalizana? Mlishaachana na mimba alishatoa. Acha kumuendekeza, mwambie ajiuguze mwenyewe
 
Babu jinga Wa wapi wewe?embu amka!kama una ela nyingi peleka kijijini kwenu au Kwa wazazi wao watashukuru sana!funga njia zote za mawasiliano naye milele!
 
Acha ngono zembe
b46f3cf256811354fc6b0a0d3db8a308.jpg
 
aaah, joseverest mkuu! mbona nlianza kutuma mimi, na nikajiona wa kwanza, sasa nashangaa reply yako ndio ya kwanza yangu ya pili, huwa unafanyaje mkuu!!!!
Hata mimi mkuu nimetuma kawaida tu..sijajua imekuwaje
 
Next time ukiwa unafanya kaa na kopo pembeni ukiona nao linakuja Likinge
 
Back
Top Bottom