Milton Mahanga: Tujenge mifumo ya utawala

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Kutoka Milton Mahanga.
TUJENGE MIFUMO YA UTAWALA

Tumesema mara nyingi kwamba kitu kinachoharibia utawala wa awamu ya tano ni kutoacha masuala ya nchi yaendeshwe kwa mifumo iliyowekwa kikatiba na kisheria. Badala yake maamuzi mengi yanafanywa kwa matakwa ya viongozi. Hii imeleta na itaendelea kuleta migongano mingi ya mihimili na mamlaka za nchi, na kuwachanganya wananchi.

Jana hadi leo Polisi na BASATA waliona kwamba wimbo wa WAPO ulioimbwa na msanii Nay Wa Mitego hauna maadili na msanii huyo akakamatwa na kuwekwa ndani na wimbo huo kufungiwa. Baadaye leo Rais akaamua kwamba wimbo huo hauna tatizo la kimaadili na hivyo uendelee tu kupigwa.

Hii ni moja ya mifano ya kutofuatwa kwa mifumo ya kiutawala hapa nchini. Kwa mfano katika jambo hili wananchi wanajiuliza nani mwenye mamlaka ya kuamua ni wimbo upi una maadili na upi hauna. Je, ni Rais au Polisi au BASATA?

Wimbo wa Nay Wa Mitego wa WAPO umeruhusiwa na Rais, je, nyimbo zingine zitakazopigwa kuanzia sasa hata kama Polisi na BASATA wataona hazina maadili, itabidi waende Ikulu kwanza kumchezea Rais na yeye ndiye aamue? Ni vizuri tukajua.
 
Back
Top Bottom