Millya kupewa kadi ya Chadema kijijini kwao

Baba Jotham

Member
Mar 6, 2012
84
40
SIKU moja baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Arusha, James ole Millya kutangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama hicho na kuhamia Chadema, chama hicho cha upinzani kimemwandalia utaratibu maalumu kwakushirikiana na wananchi ili kumkabidhi kadi ya uanachama kijijini kwao.
Akizungumza na gazeti hili jana mkoani hapa, Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema kwa sasa viongozi Mkoa wa Arusha, wanafanya mawasiliano na viongozi wa chama hicho kutoka Mkoa wa Manyara na wilayani Simanjiro, juu ya kuweka mazingira ya kumpatia kadi hiyo ndani ya wiki hii.
Alisema Millya mwenyewe anapenda kukabidhiwa kadi hiyo katika kijiji alikozaliwa, Naisinyai wilayani Simanjiro, huku wenyeji wake wakishuhudia tendo hilo.
Golugwa alisema lengo la kutaka kukabidhiwa kadi kijijini alikozaliwa, Millya amelichagua kutoka moyoni mwake na amekuwa akitamani kupewakadi huku ndugu, jamaa na marafiki, washuhudie.
Alisema chama hicho kimeona ni vema wakasaidiana na wenzao Simanjiro na Manyara kuandaa hafla ya kumkabidhi kadi huku wananchi wakishuhudia tendohili.
Aidha, aliwaondoa wasiwasi wanachama na wakazi wa Arusha na Tanzania, kuhusu kupokea wanachama wa CCM, kuwa waondoe hofu sababu chama kipo makini na kimejiandaa kwa kila mapambano.
Alisema hata siku moja katika ngome yao hataweza kupenya mamluki au fisadi yoyote na kukivuruga chama, sababu ngoma hiyo wanaicheza wenyewe na utaratibu wa uongozi ndani ya chama upo wazi mtu hapewi uongozi, na ni lazima achunguzwe kwa muda mrefu na kukubalika na wanachama wote.
Naye Mjumbe wa Baraza la UVCCM na Mwenyekiti wa Umoja huyo wilayani Arumeru, Kennedy Mpumilwa, alisema Millya ametumia haki yake kikatiba kwenda chama anachopenda.
Millya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa tangu mwaka 2008, alijiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya CCM
 
Ole millya angekabidhiwa hy kadi pale orkesumet kabisa kule sendeka anakotanuaga kifua na kutembea kama mfalme ihali pale landanai kwao hata choo ategemea cha jirani!
 
Hata angepewa IKULU It's not a big deal!
News ni mpinzani anapoamua kwenda CCM, kwa kuwa ccm ilikuwapo hata kabla ya vyama vingi.
swala la mwanaccm kuhamia upinzani sio issue hata kidogo kwa kuwa, ni lazima watu wahame chama tawala baada ya kuwa mfumo unaruhusu vyama vingi.
kwa hiyo kwangu mimi sio news hata kidogo mtu akihama CCM
 
Punguza jazba kijana, we are cleaning the house.
Kura moja ina umuhimu sana kwa sisi wapenda demokrasia.
Ume-mind?????
 
Hata angepewa IKULU It?s not a big deal!
News ni mpinzani anapoamua kwenda CCM, kwa kuwa ccm ilikuwapo hata kabla ya vyama vingi.
swala la mwanaccm kuhamia upinzani sio issue hata kidogo kwa kuwa, ni lazima watu wahame chama tawala baada ya kuwa mfumo unaruhusu vyama vingi.
kwa hiyo kwangu mimi sio news hata kidogo mtu akihama.
Najua itakuwa imekuuma sana ndani ya gamba lako.Kaza roho ndugu hiki ni kizazi cha SIDANGANYIKI na siyo kizazi cha ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI.
 
Acha jazba wewe!!!!!!!!!!!!kijana kafanya maamuzi sahihi kabisa.....ni democrasia
 
Hata angepewa IKULU It?s not a big deal!
News ni mpinzani anapoamua kwenda CCM, kwa kuwa ccm ilikuwapo hata kabla ya vyama vingi.
swala la mwanaccm kuhamia upinzani sio issue hata kidogo kwa kuwa, ni lazima watu wahame chama tawala baada ya kuwa mfumo unaruhusu vyama vingi.
kwa hiyo kwangu mimi sio news hata kidogo mtu akihama
Acha jazba wewe!!!!!!!!!!!!kijana kafanya maamuzi sahihi kabisa.....ni democrasia
Najua itakuwa imekuuma sana ndani ya gamba lako.Kaza roho ndugu hiki ni kizazi cha SIDANGANYIKI na siyo kizazi cha ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI.

Acha jazba wewe!!!!!!!!!!!!kijana kafanya maamuzi sahihi kabisa.....ni democrasia
 
Hata angepewa IKULU It’s not a big deal!
News ni mpinzani anapoamua kwenda CCM, kwa kuwa ccm ilikuwapo hata kabla ya vyama vingi.
swala la mwanaccm kuhamia upinzani sio issue hata kidogo kwa kuwa, ni lazima watu wahame chama tawala baada ya kuwa mfumo unaruhusu vyama vingi.
kwa hiyo kwangu mimi sio news hata kidogo mtu akihama CCM

Tume ya Katiba umenena sawa! Huyu dogo njaa zinamsumbua anafikiri anaweza kurekebisha maisha yake kwa kuitumia CCM? Siasa za kuchumia tumbo zimepitwa na wakati kesha ona hana nafasi yoyote CCM itakayo mpatia kula 2015 ndo maana kakimbilia huko tuone naona anautafuta Ubunge tu!
 
Hata angepewa IKULU It's not a big deal!
News ni mpinzani anapoamua kwenda CCM, kwa kuwa ccm ilikuwapo hata kabla ya vyama vingi.
swala la mwanaccm kuhamia upinzani sio issue hata kidogo kwa kuwa, ni lazima watu wahame chama tawala baada ya kuwa mfumo unaruhusu vyama vingi.
kwa hiyo kwangu mimi sio news hata kidogo mtu akihama CCM

Kwako news ni wanachama wa vyama vingine wanapohamia CCM?
 
Hata angepewa IKULU It’s not a big deal!
News ni mpinzani anapoamua kwenda CCM, kwa kuwa ccm ilikuwapo hata kabla ya vyama vingi.
swala la mwanaccm kuhamia upinzani sio issue hata kidogo kwa kuwa, ni lazima watu wahame chama tawala baada ya kuwa mfumo unaruhusu vyama vingi.kwa hiyo kwangu mimi sio news hata kidogo mtu akihama CCM

Wewe hesabu kuwa ushaumia, maana huitakii mema CDM, lakini ndiyo waTZ wengi wameiamini utafanya nini..
 
Tume ya Katiba umenena sawa! Huyu dogo njaa zinamsumbua anafikiri anaweza kurekebisha maisha yake kwa kuitumia CCM? Siasa za kuchumia tumbo zimepitwa na wakati kesha ona hana nafasi yoyote CCM itakayo mpatia kula 2015 ndo maana kakimbilia huko tuone naona anautafuta Ubunge tu!

ungejua ukwasi wa james millya usingemuita njaa kali.uliza arusha,
 
Back
Top Bottom