Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,117
- 4,771
Taasisi za Usalama wa taifa ni moja ya taasisi nyeti kwenye taifa lolote duniani ambapo tukiwa nje huwa tunasikia au kuambiwa kwamba wanaofanya kazi humo ni watu wenye mafunzo maalum na huwa hawajionyeshi au kujitangaza kwa watu kuhusu wanachofanya.
Leo millardayo.com na AyoTV zinae Evarist Chahali, Mtanzania anaeishi Ulaya lakini pia anasema aliwahi kufanya kazi kwenye Idara ya usalama wa taifa zamani lakini kwa sasa amestaafu.
Chahali ameandika kitabu kiitwacho SHUSHUSHU ambapo anasema ‘moja ya mahitaji makubwa ya mtu kupata kazi hii ni kutakiwa kuwa na akili ya ziada na sio akili ya kawaida tuliyozoea ambapo upatikanaji wa watu wa aina hii hupitia hatua mbalimbali’
‘Naomba ieleweke kuwa kwenye kitabu hiki sijazungumzia Idara ya usalama wa Taifa Tanzania bali nimezungumzia Idara za usalama wa taifa kote duniani kwani taaluma hii inafanana kama ilivyo Udaktari na taaluma nyingine‘
‘Kitabu kinazungumzia changamoto pia, kimsingi huko nyuma kwenye miaka ya 80 na 90 mwanzoni changamoto kubwa kwenye idara za usalama wa taifa ilikua wenyewe kwa wenyewe, yani idara ya nchi moja dhidi ya idara ya nchi nyingine… kulikua kama kuna kanuni flani zinatakiwa kuheshimiwa japo sio rasmi‘
‘Tishio kubwa kwa sasa kwa Idara za Usalama wa taifa duniani ni ugaidi wa kimataifa unaochangiwa na mwamko wa kidini wa makundi kama AL SHABAAB, ISIS, AL QAEDA na wengine…. hawa pia wanatumia Ushushushu lakini hawafuati kanuni‘
‘Nina malengo makubwa mawili yaliyofanya niandike hiki kitabu, kwanza ni kuondoa dhana potofu kuhusu taaluma hii kwamba kuna watu wanasema hawa ni Wanyonya damu, Wananyonga na kung’oa kucha, kitabu hiki hakizungumzii Idara ya usalama wa taifa Tanzania bali kinazungumzia taaluma hii duniani kwa ujumla’ – Evarist Chahali
Ukitaka kukisoma kitabu hiki unaweza kuingia chahali.com au chahalibooks.com/products/shushushu au Amazon (search: shushushu)
au kwa Tanzania unaweza kupiga 0717 331 444.
UNAWEZA KUMSIKILIZA EVARIST KWA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI